IQNA

Hafla za kuomboleza kufa shahidi Bibu Fatima Zahra zaanza Qum

12:11 - December 18, 2021
Habari ID: 3474691
TEHRAN (IQNA)- Hafla za kuomboleza kufa shahidi Bintiye Mtume Muhammad SAW, Bibi Fatima Zahra SAW, zinafanyika katika Msikiti wa Jamia wa mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.

Vikao hivyo vya maombolezo vimeanza Ijumaa usiku na vitafanyika baada ya sala za Magharibi na Ishaa kwa muda wa siku tano.

Hafla hizo zitajumuisha hotuba za Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Murtadha Suhufi na pia kutakuwa na qasida za maombolezo.

Waislamu hasa wa madhehebu ya Shia nchini Iran na maeneo mengine duniani kila mwaka katika mwezi wa Jammadul Ula hushiriki katika maombolezo ya kuuawa shahidi Bibi Fatima Zahra SAW. Msikiti wa Jamia wa Qum ni msikiti wa pili mkongwe zaidi katika mji huo.  

4021535

Kishikizo: iran qum fatima zahra as
captcha