IQNA

Askari wa Israel wawakamata watoto walopeperusha bendera ya Palestina Al Aqsa

21:52 - December 21, 2021
Habari ID: 3474703
TEHRAN (IQNA)- Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewakamata watoto watatu waliokuwa wanapeperusha bendera ya Palestina katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds(Jerusalem) Mashariki unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Imedokezwa kuwa watoto hao waliokuwa na umri wa kati ya miaka 12-13 walikamatwa na kuondolewa katika uwanja wa msikiti huo.

Aidha askari wa Israel wamemshambulia na kumkamata mfanyakazi wa Wakfu wa Waislamu  unaosimamia Msikiti wa Al Aqsa na maeneo mengine matakatifu mjini al Quds.

Hayo yanajiri wakati ambao, tovuti moja ya habari ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeripoti kuwa, baada ya mwaka 2014 yaani wakati vilipotokea vita vya siku 51 na kuuawa shahidi idadi kubwa ya watoto wa Palestina, mwaka huu wa 2021 ndio ulioshuhudia idadi kubwa zaidi ya watoto wa Kipalestina waliouliwa shahidi na Israel.

Mapigano yanayotokea baina ya Wapalestina na utawala wa Kizayuni husababisha vifo vya watu wengi wasio na hatia hasa wanawake na watoto wadogo. Watoto wa Kipalestina wanauliwa shahidi bure bilashi, hata kama hawashiriki kivyovyote vile katika mapigano hayo. Lakini pia watoto hao wanajeruhiwa, wanafanywa wakimbizi na haki zao zinakanyagwa kila leo na utawala katili wa Israel. Tab'an maisha ya tabu na majonzi wanayoishi watoto hao kutokana na kupoteza wazazi wao katika mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni ni janga jingine linalowatesa watoto wa Palestina katika umri wao wote. 

3477033

 

captcha