IQNA

Jinai Marekani

Vijana watatu wa Wapalestina wapigwa risasi nchini Marekani

11:44 - November 27, 2023
Habari ID: 3477954
VERMONT (IQNA) - Polisi wa Jimbo la Vermont waliripoti Jumapili kwamba vijana watatu wa Kipalestina walipigwa risasi na kujeruhiwa karibu na Chuo Kikuu cha Vermont.

Kulingana na polisi, vijana hao watatu ambao walikuwa Burlington kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kutoa shukrani walipigwa risasi na kujeruhiwa, ambapo hali ya mmoja wao inaripotiwa kuwa mbaya.

Inasemekana kuwa vijana hao walikuwa wakizungumza lugha ya Kiarabu na walikuwa wamevaa hafia za Kipalestina.

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa mshambuliaji huyo alikuwa mzungu na hawakutoa maelezo zaidi kuhusu ufyatuaji risasi huo.

Kwa mujibu wa vyombo vya Marekani, hali ya mmoja wa vijana hao imeboreka, lakini  wengine wawili  wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Gavana wa Burlington amelitaja tukio hilo kuwa la kusikitisha na kuongeza kuwa matukio ya aina hiyo ambayo husababisha kuongezeka uhasama na kambi mbili katika jamii hayapaswi kurudiwa.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina pia imelaani vikali kitendo hicho.

Kitambo kidogo, wakati vyombo vya habari vya Magharibi vilipokuwa vikipotosha habari kuhusu mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Gaza, Joseph Chabo, Mmarekani mwenye umri wa miaka 71, alishambulia nyumba ya mwanamke mmoja wa Kipalestina katika mji wa Chicago nchini Marekani na kumlenga kwa silaha baridi yeye na mwanawe  wa kiume mwenye umri wa miaka sita. Mtoto huyo  alifariki dunia kutokana na majeraha ya kuchomwa visu mara 26 na mama yake alipelekwa hospitali kutokana na majeraha makubwa aliyopata.

3486180

Habari zinazohusiana
captcha