IQNA

Hamas yaadhimisha mwaka wa 34 tokea Hamas iasisiwe

18:13 - December 06, 2021
Habari ID: 3474647
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuanza sherehe za maadhimisho ya mwaka wa 34 tangu kuasisiwa kwake.

Maadhimisho hayo yatafanyika kwa kaulimbiu ya "Hamas, Ngao ya Al Quds (Jerusalem) na Njia ya Ukombozi." Akizungumza Jumapili, Msemaji wa Hamas Fawzi Barhoum, amesema maadhimisho hayo yatajumuisha mikutano na familia za mashahidi, wafungwa, mazoezi ya kijeshi, misaada kwa jamii na mikutano na waandishi habari.

Kwa mujibu wa Barhoum, kaulimbiu ya "Hamas, Ngao ya Al Quds (Jerusalem) na Njia ya Ukombozi" ina lengo la kukumbusha kuhusu ushindi na mapambano ya Wapalestina na Hamas, hasa Brigedi ya Quds ambayo imevunja ile dhana kuwa utawala wa Kizayuni hauwezi kushindwa.

Ameongeza kuwa, kwa miongo mitatu utawala wa Kizayuni wa Israel umethibitishiwa wote kuhusu maana halisi ya mapambano na jihadi.

Barhoum amesisitiza kuwa, Hamas itaendeleza mapambano yake kwa njia zote  zikiwemo za mapambano ya silaha hadi ardhi zote za Palestina zikiombolewe na haki zote za Wapalestina zirejeshwe.

Hamas iliundwa mwaka 1987 na ni harakati kubwa zaidi ya ukombozi wa Palestina. Tokea mwaka 2007, Hamas ilichaguliwa kidemokrasia kuongoza eneo la Ukanda wa Ghaza na kufuatia ushindi huo utawala haramu wa Israel uliweka mzingiro wa pande zote dhidi ya eneo hilo na pia kunzusha vita mara nne katika ardhi hiyo ni katika jitihada za kuidhoofisha Hamas. Hatahivyo njama hizo za utawala wa Kizayuni zimeambulia patupu kwani Hamas inazidi kupata nguvu na umashuhuri miongoni mwa Wapalestina.

/4018672

Kishikizo: hamas ghaza quds
captcha