
Papa aliwasili Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rafik Hariri jijini Beirut. Katika ratiba yake, anatarajiwa kukutana na viongozi wa dini, kutembelea misikiti na makanisa ya kale, kuswali katika bandari ya Beirut kwa kumbukumbu ya wahanga wa mlipuko wa mwaka 2020, na pia kufanya kikao cha faragha na Rais Joseph Aoun.
Vyanzo vya Lebanon vinasema kuwa katika ziara hii, Papa pia atakutana na Waziri Mkuu wa Lebanon na kuhutubia mkutano wa viongozi wa taifa hilo la Kiarabu.
Papa Leo amewasili Lebanon baada ya kutembelea Uturuki, ikiwa ni hatua ya pili na ya mwisho ya ziara yake ya kihistoria Mashariki ya Kati, akitoa wito wa amani katika nchi iliyotiwa kivuli na vitisho vipya vya utawala wa Kizayuni.
Viongozi wa Lebanon, taifa linalowahifadhi wakimbizi wa Kisyiria na Kipalestina wapatao milioni moja na bado likiendelea kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi wa muda mrefu, sasa wana wasiwasi juu ya kuongezeka kwa mashambulizi ya Israel katika miezi ijayo.
Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon, katika hotuba yake Ijumaa, alieleza matumaini kuwa ziara ya Papa itasaidia kukomesha mashambulizi ya Israel dhidi ya nchi hiyo.
3495581