IQNA

Maonyesho ya Qur'ani ya Tehran ni dalili ustawishaji utamaduni wa Qur'ani Iran

18:22 - April 12, 2022
Habari ID: 3475119
TEHRAN (IQNA)- Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran ni makubwa zaidi ya aina yake katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ali Reza Moaf, Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani na Etrat ameyasema hayo alipozungumza na waandish habari leo mjini Tehran na kuongeza kuwa, maonyesho hayo ni dalili ya wazi ya jitihada za Iran za kustawisha na kuimarisha utamaduni wa Qur'ani Tukufu.

Amesema maonyesho hayo ambayo yalisitishwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la COVID-19 sasa yatafanyika tena katika ukumbi kwa kushiriki watembeleaji na wenye kuonyesha bidhaa.

Moaf amesema maonyesho hayo yataanza Jumamosi tarehe 14 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendelea kwa muda wa wiki mbili.

Maonyesho hayo ya kila mwaka ya Qur'ani  yatafanyika katika Ukumbi wa Sala (Musalla) wa Imam Khomeini. Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran amesema nara na kaulimbiu ya maonyesho yam waka huu ni: "Qur'ani, Kitabu cha Matumaini na Utulivu" na yatakuwa na vitengo 45 katika eneo lenye ukubwa wa mita mraba 40,000.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran kwa lengo la kustawisha fikra za Qur'ani Tukufu na pia kushajiisha shughuli zinazohusiana na Qur'ani Tukufu.

Maonyesho yam waka 2020 na 2021 yalifanyika kwa njia ya intaneti kutokana na vizingiti vilivyokuwa vimewekwa kuzuia maambukizi ya corona nchini.

4048865

captcha