IQNA

Hija
16:21 - May 19, 2022
Habari ID: 3475265
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema inafanya mazungumzo na Saudi Arabia kuhusu kuruhusiwa kutekeleza ibada ya Hija Wairani waliopata chanjo iliyotegenezwa ndani ya Iran.

Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema jitihada zinafanyika kwa njia za kidiplomasia kushughulikia suala hili ambalo limepelekea baadhi ya Wairani waingiwe na wasiwasi kuwa yamkini wakazuia kutekeleza Ibada ya Hija pamoja na kuwa wamepata chanjo ya COVID-19.

Huku akiashiria orodha ya chanjo cha COVID-19 ambazo zimeidhinishwa na Saudi Arabia, Khatibzadeh amesema chanjo zilizotegenezwa Iran kama vile COVIran Barekat zimezingatia viwango vya juu kabisa vya afya.

Idadi kubwa ya Wairani wanaotaka kutekeleza Ibada ya Hija mwaka huu wamedungwa chanjo zilizotengenezwa Iran.

Saudia imesema mwaka huu itapokea Waislamu kutoka nje ya nchi hiyo ambao wanataka kutekeleza Ibada ya Hija baada ya kusitishwa kwa miaka miwili lakini wanapaswa kuwa wamepata chanjo tatzi za COVID-19.

Chanjo ambazo Saudia inaziafikia ni pamoja na Pfizer-BioNTech (Comirnaty), Moderna (SpikeVax), AstraZeneca, Covishield, SK Bioscience, Vaxzevria, Jansen (Johnson & Johnson), na  Sputnik V. Chanjo zingine ambazo Saudia inazikubali lakini kwa masharti maalumu ni Sinopharm, Sinovac, na Covaxin.

4057817

Kishikizo: waislamu ، hija ، iran ، saudi arabia ، covid 19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: