IQNA

Ibada ya Hija

Mahujaji wa Magharibi hawawezi tena kuelekea Hija kupitia Mashirika ya Usafiri

16:21 - June 10, 2022
Habari ID: 3475359
TEHRAN (IQNA) – Mahujaji kutoka nchi Magharibi wanaokusudia kushiriki katika Ibada ya Hija mwaka huu lazima sasa watume maombi kupitia tovuti ya serikali, Saudi Arabia ilisema.

Uamuzi huo utaondoa jukumu la mashirika ya usafiri katika mchakato huo. Baada ya miezi kadhaa ya sintofahamu miongoni mwa wanaotarajia kuwa Mahujaji katika nchi za Magharibi kutokana na ukimya wa mamlaka ya Saudia kuhusu maeneo waliyotengewa wakati wa Hija, Wizara ya Hija ya Ufalme ilithibitisha wiki hii kwamba Waislamu katika nchi  "Ulaya, Marekani na Australia" lazima wawasilishe maombi yao kupitia tovuti ya kiserikali ya Motawif.

Kufuatia mchakato huo mpya, Waislamu kutoka nchi hizo watapata nafasi zao kupitia mfumo wa "bahati nasibu ya kiotomatiki", kisha wakishinda wanaweza kutenga nafasi na kulipia usafiri wao na malazi moja kwa moja kwa serikali ya Saudia.

Uamuzi wa Riyadh unaashiria mabadiliko makubwa ya mara moja ambayo kimsingi yanaondoa mfumo wa miongo kadhaa wa kutumia mashirika ya usafiri yaliyoidhinishwa kusajili, kuweka nafasi na kulipia safari za Hajj.

Uamuzi huo pia unakuja baada ya miaka miwili ya janga la kimataifa la COVID-19 kuzuia safari ya Hija, na kulazimisha Saudia kusimamisha kwa muda na sasa imeruhusu lakini wakati huo huo impunguza idadi ya mahujaji.

Sababu haswa za serikali ya Saudia kufanya mabadiliko makubwa katika mchakato huo haziko wazi na hazijafafanuliwa, lakini inakuja wakati Ufalme huo unajaribu kuweka kudhibiti sehemu moja michakato yote inayohusiana na safari za Hija na umraa pamoja na utalii kwa kupigia debe tovuti za kiserikali zenye kutoa huduma hizo.

Waislamu wanaotaka kutekeleza ibada ya Hija ambao walikuwa wamelipia safari zao za Hija kupitia mashirika yao ya usafiri wameshauriwa na maafisa wa Saudi kutafuta kurejeshewa malipo yao. Kabla ya uamuzi huu wa Ufalme huo, bei bei ya safari ya Hija mwaka huu tayari iilikuwa imepanda kwa kiwango kikubwa na hivyo kuibua malalmiko miongoni mwa Waislamu duniani.

3479245

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :