IQNA

Ibada ya Hija

Iran yasema Saudia imekaa kimya kuhusu gharama kubwa za Hija mwaka huu

12:37 - June 07, 2022
Habari ID: 3475344
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Shirika la Hija na Ziyara za Kidini la Iran amesema maafisa wa Saudi bado hawajajibu malalamiko ya nchi kadhaa juu ya kuongezeka kwa gharama za Hija mwaka huu wa 1443 Hijria Qamaria sawa na 2022 Miladia.

Akizungumza Jumatatu mjini Tehran, Seyed Sadeq Hosseini alisema kuwa mazungumzo yamefanyika ili kupata punguzo kutoka kwa makampuni ya Saudia mwaka huu.

Huku akiashiria kupanda kwa bei, Hosseini ameongeza kuwa barua zimetumwa kwa Wizara ya Hija ya Saudi Arabia kuhusiana na suala hilo na kwamba nchi nyingine pia zimetoa malalamiko na wasiwasi wao lakini hakuna jibu rasmi la maafisa wa Saudi Arabia hadi sasa.

Mbali na kuongezeka kwa gharama za huduma, bei za bidhaa pia zimeongezeka, alisema, akibainisha kuwa kwa mfano, bei ya vyakula vya protini imeongezeka kwa asilimia 20 hadi 40.

Kwa msingi huo,  amesema Shirika la Hija la Iran linalazimika kutoza Mahujaji karibu dola 230 zaidi ya fedha walizokuwa

Baadhi ya ripoti zimetaja janga la COVID-19, kupanda kwa gharama za ndege, na mfumuko wa bei kama sababu kuu za kuongezeka kwa bei ya Hajj mwaka huu.

Saudi Arabia imetangaza kuwa itapokea Mahujaji wa kigeni kwa ajili ya Hija mwaka huu baada ya miaka miwili ya kusimamishwa kazi kutokana na janga la COVID-19.

Takwimu zinaonyesha baadhi kuna Wairani milioni 5.8 walio kwenye orodha ya kusubiri kwa ajili ya kusafiri hadi Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Hija na wamekuwa wakisubiri kwa miaka mingi zamu yao.

4062354

captcha