IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Msikiti wa New York kuimarisha usalama baada ya shambulio

23:53 - August 06, 2022
Habari ID: 3475588
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mmoja huko Paterson, jimbo la New York Marekani, umelengwa na wahalifu wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu mapema wiki hii.

Sasa viongozi wa msikiti huo wanafikiria kuimarisha usalama.

Hujuma hiyo ilitokea katika Kituo cha Kiislamu cha North Jersey siku ya Jumatatu na tukio hilo lilinaswa kwenye video ya uchunguzi.

Video hiyo inaonyesha vijana wawili waliojifunika nyuso zao wakitembea hadi ngazi za mbele za msikiti wa kituo hicho na kuingia ndani wakati wa sala. Kisha wanaonekana kuanza kuwarushia waumini mawe, kabla ya kukimbia nje na kukimbia barabarani.

Wanaohudhuria ibada katika msikiti huo wanasema tukio hilo ni la kuti wasiwasi

"Ninashukuru kwamba hali haikuwa mbaya zaidi. Umeona hali ya hivi majuzi nchini Marekani, "anasema Abdul Tafur.

Waumini wanasema kwamba wamekabiliana na aina hii ya chuki siku za nyuma. Mnamo Desemba, mwanamume mmoja aliingia msikitini kulalamika kuhusu kusikia adhana sala kila siku. Alimsukuma imamu na sasa anakabiliwa na mashtaka.

Kuhusu tukio la hivi punde, afisa wa sherifu wa Kaunti ya Passaic analinda doria wakati wa ibada za sala na kamera za usalam ziliwekwa barabarani kutazama mtu yeyote anayejaribu kuingia ndani.

“Nimechukizwa na tukio hilo. Ni jambo la kufedhehesha na la kuchukiza,” amesema mkuu wa polisi eneo hili Sheriff Richard Berdnik. "Tunafanya kazi pamoja na washirika wetu. Nakuahidi tutahakikisha tabia hii inakoma.”

Viongozi wa misikiti wanazingatia kuajiri mlinzi lakini hatua hiyo itawagharimu kiasi kikubwa cha fedha. Kwa sasa, watategemea usaidizi wa Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Kaunti ya Passaic na kamera za usalama.

Marekani imekuwa ikishuhudia ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu kutokana na vyombo vingi vya habari na wanasiasa kueneza propaganda dhidi ya Uislamu na Waislamu.

3479996

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha