IQNA

Uadui wa Israel

Sayyid Hassan Nasrallah aionya Israel kuhusu kuchimba gesi ya Lebanon Bahari ya Mediterania

14:40 - June 10, 2022
Habari ID: 3475357
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema hatua za utawale wa Kizayuni wa Israel katika eneo la machimbo ya gesi ya Karish ni ukiukaji wa mamlaka ya Lebanon na akaonya wazi kuwa hakuna shaka yoyote kuwa Hizbullah inayo uwezo wa kijeshi na kiusalama wa kumzuia adui mzayuni asichimbe mafuta na gesi katika eneo hilo.

Siku ya Jumapili iliyopita utawala wa Kizayuni ulivuka mpaka wa baharini wa Lebanon na kuweka jukwaa la gesi katika Bahari ya Mediterania ukipanga kulitumia jukwaa hilo kuchimba mafuta na gesi eneo la machimbo ya gesi la Karish lililopo kwenye maji ya ardhi ya Lebanon.

Hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni imekabiliwa na jibu na radiamali kali za viongozi wa nchi hiyo.

Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema adui asiruhusiwe kuchimba gesi katika machimbo ya Karish na akasisitiza kuwa utawala wa Kizayuni hauwezi kulilinda jukwaa hilo linaloelea majini na kuendeleza mchakato wa uchimbaji.

Sayyid Hassan Nasrallah ameendelea kueleza kwamba, Walebanon wanakabiliana na adui asiyejali wala kuheshimu maazimio ya kimataifa; na mantiki pekee aliyo tayari kuifuata ni ya utumiaji nguvu na hiyo ndiyo njia iliyoufanya utawala huo uondoke Ukanda wa Gaza.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amekumbusha kuwa maliasili ya gesi na mafuta iliyopo katika eneo la maji ya Lebanon ndio tumaini pekee lililobaki kwa ajili ya kuiokoa nchi hiyo katika uga wa kiuchumi na akaongezea kwa kusema, muqawama imara wa ndani ya Lebanon hauwezi na wala hautaweza kukaa na kufunga mikono kutazama maliasili za utajiri wa nchi hiyo zikinyakuliwa na kuporwa.

Sayyid Hassan Nasrallah amesisitiza kwa kusema: "jukumu kuu la muqawama ni kusaidia kuihami ardhi, bahari, mafuta, gesi na heshima ya Lebanon. Huu ni wajibu wa kidini, kitaifa na kijihadi".

Katika miaka ya karibuni, Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon imewasilisha mashtaka mara kadhaa Umoja wa Mataifa na kwa Baraza la Usalama la umoja huo dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kutokana na hatua yake ya kukiuka mara kwa mara mipaka ya baharini, angani na nchi kavu ya nchi hiyo.

Onyo la Rais wa Lebanon

Rais wa Lebanon Michel Aoun naye pia ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba usijaribu kuchimba gesi katika Bahari ya Mediterania kabala ya mgogoro wa mpaka wa baharini baina ya pande mbili kutatuliwa.

Rais wa Lebanon ametoa kauli hiyo baada ya meli ya kuhifadhi na kubeba gesi  (FPSO) kufika katika eneo linalozozaniwa, ambapo kampuni yenye makao yake makuu London ya Energean inapanga kuanza kuvuta gesi kutoka chini ya bahari katika eneo la Karish chini ya mkataba na utawala wa Kizayuni wa Israeli baadaye mwaka huu.

Aoun amesema amejadili kuwasili kwa meli hiyo na Waziri Mkuu Najib Mikati na kumtaka Kamanda wa Jeshi la Lebanon kumpa "data sahihi na rasmi kuhusu suala hilo."

3479239

captcha