IQNA

Jinai za Israel

Israel yaanzisha mauaji ya kimbari Lebanon, yaua watu 270

18:53 - September 23, 2024
Habari ID: 3479478
IQNA-Ndege za kivita za utawala ghasibu wa Israel zimefanya mashambulizi makali dhidi ya miji na vijiji vya Lebanon na kuua takriban watu 274.

Wizara ya afya ya nchi hiyo ilitangaza idadi ya vifo siku ya Jumatatu, ikisema "zaidi ya 1000" wengine pia wamejeruhiwa katika mashambulizi yaliyolenga maeneo kadhaa.

Waliojeruhiwa au kuuawa ni pamoja na "watoto, wanawake, na wafanyikazi wa dharura," huku ikitabiriwa kuwa idadi hiyo yaweza kuongezeka.

Vyombo vya habari vya Lebanon vimetangaza  ndege za kivita za utawala dhalimu wa Israel zilishambulia kwa mabomu miji na vijiji vyote vilivyo kwenye mpaka wa kusini.

Ndege za kivita za Israel pia zimeripotiwa kulenga maeneo ya mashariki mwa Lebanon, likiwemo Bonde la Bekaa.

Duru za Lebanon zimesema mashambulizi hayo ya anga yalilenga jumla ya maeneo zaidi ya 40 nchini Lebanon .

Wakati huo huo, Najib Mikati, kaimu waziri mkuu wa Lebanon amezungumza Jumatatu katika mkutano wa baraza la mawaziri na kusema: "Kupanuka kwa uchokozi wa Israel dhidi ya Lebanon ni mauaji ya kimbari kwa kila maana ya neno, lengo likiwa ni kuangamiza vijiji vya Lebanon."

Aidha ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama, na mataifa yenye ushawishi "kusimama upande wa haki" ili uchokozi dhidi ya Lebanon usitishwe.

Utawala ghasibu wa Israel umezidisha mashambulizi yake dhidi ya nchi hiyo tangu Oktoba 7, wakati ulipoanzisha vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imejibu mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina kwa kushambulia ngome za kijeshi za utawala huo wa Kizayuni na kwa hivyo kuonyesha uungaji mkono kwa Wagaza waliokumbwa na vita.

3490017

Habari zinazohusiana
captcha