IQNA

Harakati ya Hizbullah

Nasrallah: Lebanon haitaki vita, lakini iwapo haitapata inachostahiki, Israeli haitachimba mafuta

21:13 - July 20, 2022
Habari ID: 3475520
TEHRAN (IQNA) Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Lebanon haitaki vita, lakini iwapo haitapata inachostahiki, utawala wa Kizayuni hautaruhusiwa kuchimba mafuta.

Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah, amesema: "Tunaweza kuingia vitani na au la, hatuna hamu ya kufungua uwanja wa vita, tunataka haki zetu. Ikiwa suluhisho la baadhi ya watu nchini Lebanon ni kujisalimisha, sisi Hizbullah hatutakubali jambo hilo."

Sayyid Nasrullah ameongeza kuwa mwaka 1982 wakati Hizbullah ilipoanzishwa, ilikuwa harakati ya muqawama na mapambano kwa sababu ilikuwa tishio kwa Israel, lakini hii leo harakati hiyo sio tishio kwa Israel pekee, bali ni tishio kwa mradi mzima wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Amesema adui leo anajiona mnyonge na hataki vita kwa sababu anajua kwamba vita hivyo havitakuwa vya Hizbullah pekee na huenda vikashirikisha mhimili mzima wa mapambano na kupelekea kusambaratika kwake; kwa sababu hiyo vita ni hatari yenye gharama kubwa kwa Israel.

katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa: Marekani inatutaka tujisalimishe na kudhalilika; Inataka tukabidhi silaha zetu, kutambua rasmi utawala haramu wa Israel, iendelee kupora mali, na inaona kuwa Muqawama na washirika wake ndio kikwazo pekee kwa mipango yake.

4072236/

captcha