IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Hizbullah ilikataa hongo ya kifedha ya Marekani kusitisha makabiliano na Israel

22:15 - July 22, 2022
Habari ID: 3475525
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon anasema harakati harakati hiyo ilikataa mapendekezo kadhaa ya hongo ya kifedha ya Marekani ili kusitisha mapambano yake na utawala wa Kizayuni wa Israel .

Katika mahojiano ya aina yake yaliyorekodiwa miaka 20 iliyopita na kurushwa hewani wiki hii, Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Nasrallah anasema harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu au muqawama ilikataa mapendekezo kadhaa ya Marekani ya  fedha na kutambuliwa rasmi ili ijiondoe ijiondoe katika kadhia ya mgogoro wa Waarabu na Waisraeli.

Kanali ya Televisheni ya Al Mayadeen ya inarusha hewani  vipindi vitano  vilivyopewa anwani ya "40 na Zaidi" kuhusu harakati ya Hizbullah. Vipindi hivyo vinarushwa hewani kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa Harakati ya Hizbullah na pia  kumbukumbu ya miaka 30 ya kuchaguliwa Sayyid Hassan Nasralllah kama mkuu wa harakati. Vipindi hivyo ni ni pamoja na mahojiano yalichorekodiwa kitambo lakini ambayo hayajawahi kurushwa hewani baina ya Sayyid Nasralllah na Ghassan Ben Jeddou, Mkurugenzi Mtendaji wa sasa wa al-Maydeen.

Katika sehemu ya tatu ya vipindi hivyo, Nasrallah anasema Marekani ilitoa ofa kadhaa kwa Hezbollah baada ya ukombozi wa kusini mwa Lebanon na eneo la magharibi mwa Bekaa mnamo 2000, ikilenga kuleta mabadiliko katika harakati hio na kuiondoa kabisa katika kadhia ya mgogoro wa Waarabu na Israel.

Marekani  ikijaribu kuishawishi Hizbullah kwamba hakuna haja ya mapambano kuhusu mashamba ya Shebaa yanayokaliwa kwa mabavu na Israel na kwamba kadhia hiyo inaweza kutatuliwa kwa mazungumzo, amesema Sayyid Nasrallah.

Kwa mujibuwa wa Sayyid Nasrallah, kile ambacho Marekani ilikuwa ikitoa kwa Hizbullah mkabala wa harakati hiyo kusitisha mapambano ni  pamoja na suluhisho kuhusu suala la wafungwa wa Lebanon katika magereza ya Israel, kutambua jukumu la kisiasa la Hizbullah na kuingizwa Hizbullah serikalini, kuipa harakati hiyo misaada  ya kifedha ya kujenga tena maeneo yaliyokombolewa na kuiondoa Hizbullah kutoka kwenye orodha ya Marekani ya eti makundi ya kigaidi.

Sayyid Nasrallah pia amefichua kuwa Marekani ilikuwa inataka Hizbullah isitishe uungaji mkono wake wa kifedha na kijeshi kwa harakati za ukombozi wa Palestina.

Ameongeza kuwa Hizbullah ilikataa kabisa mapendekezo hayo ya Marekani kwani harakati hiyo ina azma ya kuendelea kuunga mkono wa Palestina na inautazama utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni tishio kwa usalama wa Lebanon.

Marekani ilikariri mapendekezo hayo kwa Hizbullah baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001 baada ya kutangaza kuanzisha vita dhidi ya makundi yote iliyoyatuambua kuwa ni ya ‘kigaidi’.

Hizbullah ilianzishwa kufuatia uvumbuzi wa Israeli dhidi ya kusini mwa Lebanon mwaka  1982  na tangu wakati huo, harakati hii imestawi kwa kasi na kupata nguvu kubwa za kijeshi na kiisasa

Hizbullah imekabiliana vita vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lebanon mara mbili,  mnamo 2000 na 2006, ambapo jeshi la utawala huo lililazimishwa kurudi nyuma kutokana na mapambano shupavu ya Hizbullah.  Harakati hiyo imeapa kutetea kwa dhati Lebanon katika vita vingine na Israel.

3479791

captcha