IQNA

Taazia

Harakati za Palestina zatuma rambirambia baada ya kuaga dunia mama mzazi wa Sayyid Nasrallah

21:34 - May 26, 2024
Habari ID: 3478885
IQNA - Makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina yametuma salamu za rambirambi kwa Katibu Mkuu Sayed Hassan Nasrallah kwa kuondokewa na mama yake mzazi.

Hizbullah ilitangaza kifo cha Umm Hassan katika taarifa siku ya Jumamosi, ikibainisha kwamba aliaga dunia baada ya kuhangaika na ugonjwa.

Harakati hiyo ilimtaja marhuma Umm Hassan kama "mama mwaminifu na mtakasifu, ambaye alilea na kukuza familia iliyojitolea, yenye bidii, na yenye heshima."

Iliwaalika wanachama na wafuasi wa harakati hiyo kushiriki katika msafara wa mazishi yake kwenye Makaburi ya Mashahidi katika mji mkuu Beirut siku ya Jumapili.

Muda mfupi baadaye, Ismail Haniyah, mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Wapalestina , Hamas, yenye makao yake Ukanda wa Gaza, Hamas alitoa salamu za rambirambi kwa kiongozi wa Hizbullah kutokana na msiba huo

"Kwa huzuni kubwa..., tumepokea taarifa za kufariki kwa mama yako mtukufu, Umm Hassan Nasrallah," Haniyah alisema katika ujumbe.

"Tunakukabidhi  salamu zetu za rambirambi, wakati huu ambapo ndugu zetu huko Lebanon wanasimama kwa mshikamano na ndugu zao huko Palestina," iliongeza taarifa hiyo, ikiashiria uungaji mkono wa Hizbullah kwa mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala wa Israel.

Kundi la Jihad Islami lenye makao yake makuu huko Gaza, pia limetoa "rambirambi za dhati na masikitiko" kwa mkuu wa Hizbullah.

Kamati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina, ambayo ni muungano wa makundi kadhaa ya muqawama wa Palestina, na tawi lake la kijeshi la al-Nasser Salah al-Deen Brigades pia zimetuma salamu za rambi rambi kwa kiongozi wa Hizbullah.

3488503

Habari zinazohusiana
captcha