IQNA

Waislamu Italia

Msikiti wa kwanza katika mji wa Venice nchini Italia wazinduliwa

17:05 - June 12, 2022
Habari ID: 3475369
TEHRAN (IQNA) - Msikiti wa kwanza huko Venice, Italia, ulizinduliwa katika hafla iliyohudhuriwa na wawakilishi wa jamii ya Kiislamu ya Italia na taasisi za jiji.

Ufunguzi wa msikiti huo unamaanisha mji – mji wa Venic ambao ni uko katika Orodha ya UNESCO ya Turathi za Dunia na ambao pia ni nembo ya utalii na sanaa - sasa ina mahali maalum pa ibada kwa maelfu ya Waislamu wanaoishi katika eneo hilo.

Jengo hilo lilinunuliwa na jamii ya Waislamu kutoka katika fedha za Zaka iliyokusanywa na Waislamu wa Venice na bandari ya karibu ya viwanda ya Mestre.

"Ninatumai kuwa kuanzia sasa watalii wanaokuja kutoka kote ulimwenguni watakapotembelea Venice, watachukua nyumbani sio kadi ya posta ya jiji tu bali pia ya msikiti huu, msikiti wa Venice," amesema Yassine Lafram, rais wa Jumuiya ya Kiislamu ya Bologna ambaye pia ni rais wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Italia.

"Tunajivunia eneo hili, kwa kuwa ni ushahidi zaidi wa ushirikiano wetu."

Roberto Berton na Nandino Capivilla wakiwakilisha jimbo kuu la Kikatoliki walihudhuria hafala ya ufunguzi ambayo pia iliwashirikisha madiwani kadhaa wa manispaa na wanasiasa wa eneo hilo.

"Msikiti huu wa Venice sasa uko wazi kwa kila mtu kutokana na katiba ya Italia, ambayo inaruhusu kila raia kusali Mungu amtakaye na popote anapotaka kufanya hivyo," Lafram aliongeza.

Rais wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu Italia alisema kuwa Waislamu wote wanaoishi Italia wanataka kusaidia "kuunda nchi ambayo kila mtu anaheshimiwa na kufanya kazi kwa manufaa ya wote."

Alisema msikiti huo mpya hauna mpango wa kuwa "mahali pamefungwa, wazi kwa Waislamu pekee."

Aliongeza kuwa: “Msikiti huu unaofunguliwa katika jiji lenye tamaduni nyingi unaotembelewa kila siku na watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia, utatoa uhai kwa shughuli nyingi ambapo kila mtu atakaribishwa. Kuanzia sasa, mahali hapa patakuwa wazi kwa wote, hasa taasisi za eneo la Venice."

"Tuko wazi kwa miradi yoyote, tafiti na masomo kuhusu utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu na ushirikiano," amemsema na kuongeza kuwa mji wa Venice umestahiki kuwa na msikiti.

3479264

captcha