IQNA

Chama cha misimamo mikali Italia kuchunguzwa kuhusu picha za Chuki dhidi ya Uislamu

22:19 - April 19, 2025
Habari ID: 3480561
IQNA – Chama kimoja cha misimamo mikali ya mrengo wa kulia nchini Italia, kinachoongozwa na Naibu Waziri Mkuu Matteo Salvini, kinahunguzwa rasmi baada ya wabunge wa upinzani kuwasilisha malalamiko kuwa chama hicho kimesambaza picha zinazozalishwa na Akili Bandia (AI) zinazokuza ubaguzi wa rangi na dhana za Chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia.

Malalamiko hayo, yaliyowasilishwa kwa mdhibiti wa mawasiliano wa Italia Agcom siku ya Alhamisi na wanachama wa Chama cha Kidemokrasia na Muungano wa Kijani na Kushoto, yanashutumu chama cha The  League kwa kusambaza maudhui yanayohusisha aina nyingi za hotuba za chuki kupitia majukwaa yake ya mitandao ya kijamii. 

Kwa muda wa mwezi uliopita, picha nyingi zinazozalishwa na AI zilichapishwa kwenye akaunti rasmi za League, zikionyesha watu wasio wazungu, aghalabu wakiwa na silaha  na katika hali za vurugu au jinai. 

Kwa mujibu wa Seneta wa Chama cha Kidemokrasia Antonio Nicita, picha hizo zinalenga wahamiaji hasa Waafrika  na Waarabu, zikionesha kuwa wao ni tishio kwa usalama wa umma. Alisema chama kilitumia akili mnemba "kujenga simulizi zinazohusisha makundi fulani ya kikabila au kidini na tabia za jinai."

Emilio Borrelli, mbunge wa Muungano wa Kijani na Kushoto, alielezea maudhui hayo kama chombo cha "kupandikiza hofu na kuhamasisha chuki," akisisitiza wasiwasi kwamba ujumbe kama huo unaweza kuchangia kuimarisha mitazamo ya chuki katika umma. 

Msemaji wa League alikubali kwamba baadhi ya picha zilikuwa zimezalishwa kidigitali lakini akatetea hatua za chama, akidai machapisho hayo yalitokana na a habari halisi.  

Hata hivyo, wataalamu wa picha za kidigitali wamepinga maelezo hayo. Wachunguzi wa uchunguzi waligundua kwamba picha hizo zina dalili za wazi kuwa ni za AI, na licha ya miongozo ya maudhui ya EU, picha nyingi hazikuwa na lebo sahihi.

Picha moja maalum iliyotajwa katika malalamiko inaonyesha wanandoa waliovaa mavazi ya Kiislamu wakionekana kumnyanyasa mtoto , taswira ambayo wakosoaji wanasema inakuza dhana za chuki dhidi ya Uislamu. Hata hivyo, makala ya habari iliyotajwa katika maandishi ya maelezo ya picha haikutoa maelezo kuhusu dini au kujumuisha picha yoyote inayohusiana. 

Mzozo huu unatokea katikati ya mwelekeo mpana barani Ulaya, ambapo vikundi vya mrengo wa kulia i vinatumia zaidi picha zinazozalishwa na AI kueneza chuki dhidi ya wahamiaji hasa Waislamu.

 

349273

captcha