Picha hiyo ilipigwa huko Jabalia, kaskazini mwa Gaza, wakati wa mzingiro wa mwezi mmoja wa utawala wa Israel katika eneo hilo huku kukiwa na mashambulizi makali ya utawala huo dhalimu.
Picha hiyo, iliyoripotiwa kuchapishwa kwenye akaunti ya kibinafsi ya Instagram ya mwanajeshi kutoka Brigedi ya Givati 435 ilisambazwa kuanzia tarehe 22 Oktoba 2024.
Tukio hilo limechochea ghadhabu mtandaoni, huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakilinganisha hali dhahania zinazohusisha maandishi mengine ya kidini. Iwapo jambo kama hilo lingehusi vitabu vya dini zingine lingekosolewa lakini kwa ajili ni Qur'ani Tukufu limenyamaziwa kimya.
"Ikiwa mtu atachapisha picha inayodharau Torati, kungekuwa na lawama nyingi. Lakini wakati wanajeshi wa Israeli wanapochapisha picha zinazoidhalilisha nakala za Qur'ani na misikiti, hakuna lawama, zaidi ya kusifiwa kwao kama jeshi lenye maadili zaidi duniani,” mtumiaji mmoja aliandika, kulingana na The New Arab.
Wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina wameandika matukio kadhaa ya kuvunjiwa heshima Qur'ani na wanajeshi wa Israel, ikiwa ni pamoja na kuteketeza moto nakala za Qur'an.
Mwezi Mei, shirika la utangazaji la Kizayuni Kan liliripoti kuhusu tukio ambapo mwanajeshi alichoma moto nakala ya Qur'ani katikati ya magofu ya msikiti mmoja huko Gaza.
Kuvunjiwa heshima maeneo ya ibada na nembo za kidini kama vile nakala za Qur'ani Tukufu kunapingana na Kifungu cha 27 cha Mkataba wa Hague wa 1907, unaowataka wanajeshi “kuhifadhi, kadiri inavyowezekana, majengo yaliyowekwa kwa ajili ya dini.” Hata hivyo, vikosi vya Israel vinakaidi sheria za kimataifa vinaendelea kuharibu maeneo ya kidini na kitamaduni huko Gaza na kwingineko.
Tangu kuanza kwa hujuma ya Israel dhidi ya Gaza Oktoba mwaka jana, Wapalestina wasiopungua 43,922 wameuawa shahidi na 103,898 kujeruhiwa huko Gaza, huku watu 3,481 wakiuawa na 14,786 kujeruhiwa huko Lebanon katika hujuma za Israel katika kipindi hicho.
3490739