IQNA

Turathi za Kiislamu

Jumba la Makumbusho la Benaki laonyeshaSanaa ya Kiislamu Barani Ulaya

12:08 - July 14, 2022
Habari ID: 3475501
TEHRAN (IQNA) – Jumba la Makumbusho la Benaki huko Ugiriki lina mkusanyiko wa kazi za sanaa zilizokusanywa zaidi ya karne 13, nyingi zikiwa na umuhimu maalum.

Baadhi ya vitu katika jumba hili la makumbusho, ambavyo vilikusanywa na "Antonis Benakis", mwanzilishi wa jumba hilo la makumbusho, katika miongo ya kwanza ya karne ya 20, ni vya thamani zaidi kuliko mkusanyiko wa turathi za Kiislamu katika majumba muhimu ya makumbusho lama vile Louvre huko Paris  na Jumba la Makumbusho la London.

Antonis Benakis, Jumba la Makumbusho la Benaki, ambaye alijua umuhimu wa utamaduni wa Kiislamu na alipenda kazi hii, tangu 1976, alijitolea kukusanya turathi za Kiislamu na kujenga mkusanyiko tofauti ili kuwasilisha sanaa ya Kiislamu, mpaka hatimaye aliweza kutayarisha na kufungua kituo hiki mnamo Oktoba 2004.

Eneo la jumba hili la makumbusho lina zaidi ya mita za mraba 1000 na limeunda uwezekano bora wa kuonyesha zaidi ya vipande 8000 vya kauri, kazi za chuma, dhahabu, uchongaji, fuwele, nguo na kila aina ya mawe na silaha zinazohusiana na enzi ya mwanzo wa Uislamu.

Kwenye ghorofa ya kwanza, turathi kutoka enzi ya kwanza ya Kiislamu - karne ya 7 hadi 12 – Miladia zinaonyeshwa, na ghorofa ya pili imejitolea kwa sanaa za Kiislamu katika enzi ya karne ya 12 hadi 16 miladia. Kwenye ghorofa ya tatu, mawe ya ajabu ya marumaru, yanayohusiana na majumba ya karne ya 17 ya Cairo, pamoja na hazina nzuri kutoka Uturuki na Iran, hutembelewa na wale wanaopenda.

Kwenye ghorofa ya mwisho ya jumba hili la makumbusho, vitu vya sanaa baada ya karne ya 19, ambavyo ni pamoja na mkusanyiko wa silaha na vito vya thamani vya Iran kutoka enzi ya Qajar, vinaonyeshwa.

Miongoni mwa kazi hizo, kauri za Kiirani za karne ya 17 kutoka katika jumba la makumbusho la "Victoria na Albert" huko London na vilevile nakala za kale za Qur'ani Tukufu au Misahafu iliyoandikwa kwa mkono, ni mashuhuri zaidi.

Mkusanyiko wa vito vya jumba hili la makumbusho pia unajumuisha vipande 500 vya vito kama vile pete, shanga, bangili na mikanda.

Mkusanyiko wa kuchonga una vipande 700, ambavyo vingi ni vya Misri. Katika sehemu hii, kuna kazi kutoka Iran ya kale na maeneo mengine ya ulimwengu Kiislamu, ambazo inaonekana zaidi na maumbo ya kijiometri.

Mkusanyiko wa porcelaini na glasi pia unajumuisha vipande 700, ambavyo vingi vimevunjika na mabaki yanaonyesha historia ya utengenezaji wa glasi wa Kiislamu. Nyingi ya makusanyo haya ni ya zama za mwanzo na za kati za Uislamu.

3479690

captcha