IQNA

Turathi za Kiislamu

Misahafu Adimu, Hati Za Kale Zinazoonyeshwa Katika Maonesho ya Bradford

17:16 - January 21, 2025
Habari ID: 3480087
IQNA – Mkusanyiko wa misahafu adimu na hati za kale sasa umeonyeshwa katika maonesho ya "Kuhangaika Kusikika" katika Jumba la Sanaa la Cartwright Hall huko Bradford, yanayofanyika hadi Aprili 27.

Maonesho haya yanaonyesha  mkusanyiko wa athari mbali mbali kutoka Maktaba ya Uingereza, ambapo aghalabu ya athari hizo ni zilionyeshwa kaskazini mwa Uingereza kwa mara ya kwanza.

Miongoni mwa vitu muhimu ni msahafu kutoka karne ya 9, ukiwa na umri wa zaidi ya miaka elfu moja, na msahafu wa karne ya 19 uliotafsiriwa katika Kichina, The Telegraph & Argus liliripoti Jumanne.

Pia kumeonyeshwa hati ya Kiurdu kutoka mwaka wa 1590, ikitoa mwangaza juu ya urithi wa fasihi wa eneo hilo.

Maonesho haya yameandaliwa pamoja na Bingwa wa Dunia wa Ndondi Tasif Khan, washiriki wa taasisi yake ya ndondi, na mchoraji wa hati za kiarabu Razwan Ul-Haq.

Akiwa anaongea kuhusu maonesho hayo, Ul-Haq alisisitiza uzoefu wa kipekee unaowasubiri wageni: "Yatakaleta ni hisia za kushangazwa, kufurahi, kushangaa, na heshima."

3491545

Kishikizo: turathi za Kiislamu
captcha