IQNA

Turathi za Kiislamu

Mamufti wa Kyrgyzstan watembelea maonyesho ya turathi za Kiislamu Makka

21:34 - December 17, 2024
Habari ID: 3479912
IQNA - Mufti na naibu mufti wa Kyrgyzstan wameonyesha kuvutiwa kwao na turathi za kitamaduni na katika maonyesho huko Wilaya ya Utamaduni ya Hira huko Mecca. 

Sheikh Abdulaziz Zakirov na naibu wake, Sheikh Joldoshbek Abdyldaev, walikuwa katika ziara ya wilaya hiyo.

Wakati wa ziara hiyo, Zakirov na Abdyldaev waliguswa sana na Maonyesho ya  Wahyi. 

Maonyesho hayo yanatoa maelezo ya kipekee wa hadithi za manabii, kuanzia Adamu hadi Muhammad. Kitu muhimu ni uhuishaji wa ndani wa Pango la Hira, ambapo Nabii Muhammad SAW alipokea Wahy wake wa kwanza. 

Pia yanaonyesha vitu vya thamani, ikiwa ni pamoja na kopi ya nakala ya Qur'ani iliyowahi kumilikiwa na Sahaba Uthman ibn Affan na maandiko ya mawe ya kale yenye aya za Qur'ani. 

Mufti na naibu mufti wa Kyrgyzstan walipongezajuhudi katika wilaya hiyo za kukuza ufahamu na uelewa miongoni mwa wageni wa kimataifa.

Maonyesho hayo yako karibu na Jabal Al-Noor maarufu kama Wilaya ya Utamaduni ya Hira. Hilo ni eneo muhimu la turathi na ni kivutio cha kimataifa, chenye maarifa kuhusu historia na mila za Kiislamu kwa waumini wanaotemelea Makka.

3491075

Habari zinazohusiana
captcha