IQNA

Mfumo wa kifedha wa Kiislamu

Benki ya Kwanza ya Kiislamu ya Australia kufunguliwa

18:51 - July 13, 2022
Habari ID: 3475496
TEHRAN (IQNA) – Benki ya kwanza ya Kiislamu ya Australia imeidhinishwa kuwa na leseni yenye masharti ya kuchukua amana chini ya Sheria ya Benki.

Mamlaka ya Udhibiti wa Taasisi za Kifedha Australia (APRA) imeidhinisha rasmi benki kupokea leseni.

Benki ya Kiislamu ya Australia itatoa huduma za benki ambazo zinatii Sheria za Kiislamu kwa idadi ndogo ya wateja kuanzia 2023.

Sheria za Kiislamu zinawapa Waislamu seti pana ya kanuni za kuishi maisha ya kimaadili. Kulingana na imani za Kiislamu, kutumia bidhaa zinazopata au kulipa riba ni marufuku kwa sababu kunaonekana kuwa ni unyonyaji, ukandamizaji na dhuluma. Kwa mfano, kutozwa riba kwa mkopo mdogo unaohitajika ili kukidhi mahitaji ya kimsingi ya kifedha kunachukuliwa kuwa sio sawa.

Katika mfumo wa benki wa Australia, riba inatekelezwa kila mahali, na kufanya kuwa vigumu kwa asilimia 3.2 ya Waaustralia wanaojitambulisha kuwa Waislamu kufuata sheria zao wenyewe.

Hapo ndipo Benki ya Kiislamu ya Australia inapokuja, ili kutoa chaguo zinazotii Uislamu kwa wale wanaotaka.

Ingawa benki za Kiislamu sio dhana mpya. Kuna mamia ya benki zinazochukua amana kote ulimwenguni ambazo zinatii sheria za mfumo wa kifedha wa Kiislamu. Benki ya Kiislamu ya Australia imekuwa ya kwanza nchini Australia.

Awali, Benki ya Kiislamu ya Australia itatoa huduma ya akaunti za kila siku, amana za muda na mikopo ya nyumba. Itafanya kazi kama benki nyingine yoyote. Tofauti kuu ni kwamba hakuna kitu kitakachopata riba.

Badala ya bidhaa za kawaida za kupata riba, Benki ya Kiislamu ya Australia itatoa mtindo wa kukodisha-kununua kwa mikopo ya nyumba.

Kufikia sasa, benki bado haijafunguliwa kwa biashara. Kwa leseni yake ya sasa ya APRA iliyowekewa vikwazo, Benki ya Kiislamu ya Australia inaweza tu kuwa na idadi ndogo ya wateja mwaka ujao 2023. Benki hii inatarajia kupata idhini ya APRA ili kutoa bidhaa zake kwa umma kwa jumla ifikapo 2024.

3479691

captcha