IQNA

Ibada ya Umrah

Kundi la kwanza lawasili Makka kwa ajili ya Umrah

19:21 - July 31, 2022
Habari ID: 3475563
TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Urais Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitukufu ya Makka na Madina imepokea kundi la kwanza la Waislamu waliongia Saudia kutekeleza ibada ya Hija ndogo ya Umrah Jumamosi.

Hapo awali matayarisho yalikuwa yamekamilika kwa ajili ya kupokea kundi la kwanza la Waislamu wanaotekeleza ibada ya  Umra baada ya kukamilika msimu wa Hajj mwaka 2022.

Afisa mtendaji katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Osama Al-Hujaili amesema kuwa Mataf (eneo la kuzungukia Al-Kaaba Tukufu) katika Msikiti Mkuu na ghorofa ya chini zilitengwa kwa ajili ya wanaofanya Umra. Wakati ghorofa ya kwanza ya Mataf ilitengwa kwa ajili ya waumini ambao hawafanyi Umrah.

Wiki iliyopita, Mamlaka ya Saudia inasema wanaoshiriki katika Hija ndogo ya Umrah wanahitaji kuvaa barakoa kwenye Msikiti Mtakatifu wa Makka kama hatua ya tahadhari kufuatia kuongezeka maambukizi ya COVID-19.

Wizara ya Hija na Umrah ya Ufalme wa Saudi Arabia ilitangaza kuwa ni sharti kwa wenye kushiriki ibada a Umrah kuthibitisha kuwa wana afya njema kupitia apu ya simu za mkononi ya  Tawakkalna na kuvaa barakoa usoni wakati wote wa kuwepo kwenye Msikiti Mtakatifu wa Makka.

Waumini hao pia wanatakiwa kuondoka msikitini baada ya kumalizika kwa muda waliotengewa  kuingia na kuepuka kuingiza mizigo katika eneo hilo wakati wa ibada.

Msimu mpya wa Umrah umeanza siku ya kwanza ya Muharram, mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu ambao katika aghalabu ya nchi ulianza Julai 30.

Mnamo Oktoba 2020, Saudi Arabia polepole ilianza tena Umrah baada ya takriban miezi saba ya kusimamishwa kwa sababu ya janga la kimataifa la COVID-19.

Waislamu ambao hawawezi kushiriki katika ibad aya Hija ya kila mwaka kwa kawaida hutekeleza  Umra katika Msikiti Mtakatifu wa Makka.

3479912

Kishikizo: waislamu umrah saudia
captcha