IQNA

Ibadah ya Umrah

Waislamu Milioni 3 wamesali ndani ya Rawdah katika kipindi cha miezi mitatu

12:53 - November 10, 2022
Habari ID: 3476067
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa takwimu, zaidi ya Waislamu milioni tatu wameswali katika Rawdah Tukufu kwenye Msikiti wa Mtume (SAW), Al-Masjid an-Nabawi , mjini Madina katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu wa 1444 Hijria Qamaria.

Rawdah Tukufu iko kati ya Chumba Kitukufu (kinachojulikana kama nyumba ya Mtume), na Minbar ya Mtume Muhammad (SAW). Sehemu hii ya kusini-mashariki ya Al-Masjid an-Nabawi ndipo nyumba ya mtukufu huyo iliposimama, ambapo aliishi na kuzikwa. Ni ya thamani kubwa sana ya kidini kwa Waislamu.

Kati ya waumini hao, 2,273,033 walikuwa wanawake na 1,149,364 walikuwa wanaume, vyombo vya habari vya Saudia viliripoti Jumatano.

Jumla ya waumini 4,125,257 waliofika hapo kwa ajili ya Hija ndogo ya Umrah pia walitoa heshima zao kwa Mtume Muhammad SAW na masahaba zake wawili Abu Bakr Al-Siddiq na Umar ibn Al-Khattab.

Halikadhalika milo 825,000 ya futari ilitolewa kwa wageni wa Al-Masjid an-Nabawi katika kipindi hicho na waumini milioni 1.2 walinufaika na huduma za tafsiri katika lugha kumi tofauti ambazo zilitolewa kupitia tovuti zilizo eneo hilo.

Mwaka wa sasa wa Hijri ulianza tarehe 30 Julai 2022.

3480079

Habari zinazohusiana
captcha