IQNA

Umrah

Saudi Arabia yaanza tena kutoa visa za Umrah

16:46 - July 16, 2022
Habari ID: 3475511
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Hija na Umra ya Saudi Arabia ilitangaza kurejesha utoaji wa visa za Umrah baada ya kusitishwa wakati wa msimu wa Hija.

Wizara hiyo ilisema katika taarifa yake kwamba imeanza kutoa visa kwa Waislamu kutoka nje ya Saudi Arabia walio tayari kufanya Hija ndogo ya Umra na kutembelea Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina.

Taarfia hiyo Hija ndogo y Umrah itaanza tena siku ya kwanza ya mwezi wa Hijri wa Muharram, ambao unatazaiwa kuangukia Julai 30.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maombi ya visa ya Umra yanapaswa kufanywa kupitia Apu ya Eatmarna.

Wizara ya hiyo ya Saudia ilikuwa imesimamisha Umrah mnamo Juni 24.

Hija ndogo ya Umra ni safari ya kwenda Makka ambayo Waislamu wanaweza kuitekeleza wakati wowote wa mwaka, tofauti na Hija asili ambayo inapaswa kufanyika tu katika siku za kwanza za mwezi wa  Dhul Hajja.

Mwaka huu, Mahujaji milioni moja kutoka nchi mbalimbali walishiriki katika ibada ya Hija.

Msimu wa Hija ulianza Julai 1, ukiashiria msimu wa kwanza wa Hija baada ya janga baada ya miaka miwili ya usumbufu mkubwa uliosababishwa na COVID-19.

4070938

captcha