IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Marekani

Misikiti huko Houston Marekani kuimarisha usalama kufuatia mauaji ya Waislamu wanne

23:21 - August 09, 2022
Habari ID: 3475600
TEHRAN (IQNA) - Hatua za usalama zinatarajiwa kuimarishwa karibu na misikiti huko Houston Marekani baada ya wanaume wanne Waislamu kuuawa ndani ya siku 10 huko Albuquerque.

Wakati uchunguzi wa mauaji haya ukiendelea, maafisa wa kutekeleza sheria kama Mkuu wa Polisi wa Houston Troy Finner na Meya Sylvester Turner tayari wameimarisha doria zaidi karibu na misikiti.

Jumuiya ya Waislamu wa Houston iko imara, na takriban asilimia 11 ya wakazi wa jiji hilo wakijitambulisha kuwa Waislamu, lakini mashambulizi dhidi ya jumuiya yamekuwa yakitokea tangu 2001.

"Nyumba za Waislamu zimelengwa kwa risasi, msikiti ulipigwa risasi huko Katy," alisema William White, mkurugenzi wa Baraza la Mahusiano ya Kiislam na Marekani huko Houston. "Kumekuwa na vichwa vya nguruwe vilivyoachwa kwenye milango ya mbele ya msikiti, kumekuwa na barua za hasira au barua za chuki zilizotumwa kwa wanajamii wa Kiislamu, nyumba na magari. Na kumekuwa na hali ya hofu kwa miaka 21 iliyopita."

Jumuiya ya Waislamu huko Houston imedumisha uhusiano mzuri na viongozi waliochaguliwa wa eneo hilo, White alisema, lakini pia aliongeza kuwa hofu inabaki kwa jamii ya eneo hilo.

Viongozi wengine wa Kiislamu, kama Imam Mohammad Ahmad Khan katika Fort Bend, anazungumzia hali ya Waislamu Houston na kusema "Wakati mwingine, unapokuwa katika maeneo ambayo idadi ya Waislamu sio kubwa, na haijaunganishwa vizuri, inaweza kuwa changamoto zaidi."

Imam Ahmad pia aliongeza kuwa aina hii ya mashambulizi yanaifanya ionekane kama jamii nzima ya Kiislamu iko hatarini.

White sasa anapendekeza wakazi wa Kiislamu kuwa waangalifu  zaidi na kuongeza, "Tunawasihi wanajamii kuwa waangalifu siku nzima wanapohudhuria msikiti, wanapohudhuria maeneo ambayo yanaweza kuwa yanahusishwa na Waislamu, kama vile maduka ya vyakula vya Halal, kama vile migahawa ya Kiarabu, Kusini mwa Asia."

Maeneo mbali mbali ya Marekani yameshuhudia ongezeko la hujuma za wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

3480026

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha