
Wanafunzi hao waliripoti kuwa mnamo Novemba 18, wanaume wasiojulikana walikabiliana nao wakati wa tukio lao la kila mwezi la sala ya alfajiri.
Mkusanyiko huo, uliofanyika saa 12 alfajiri (6:00 asubuhi) juu ya jengo la maegesho la Collins Parking Garage, uliandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Waislamu (MSA) na umekuwa ukifanyika kwa miezi kadhaa bila matatizo.
Saajid Khan, mwanachama wa MSA, alieleza tukio hilo kuwa la kusikitisha sana. Alisema wanaume hao walikaribia wakati wa sala na kuanza kupiga kelele kwa hasira.
Kwa mujibu wa Tampa Bay 28, Khan alisema walitoa matusi, kelele na maneno ya dharau dhidi ya dini ya Kiislamu.
Aliongeza kuwa wanaume hao walikaribia wanafunzi, wakawaelekeza kamera na kuwapiga kelele wakiwa katika ibada. Mmoja wao, akiwa amevaa buti nzito, aliwazunguka huku akipiga hatua kwa nguvu, jambo lililowatia hofu waliokuwepo.
Wanafunzi walisema pia kuwa wanaume hao walielekeza kamera kwa imamu aliyekuwa akiongoza sala na kuendeleza vitendo hivyo hadi mwisho wa ibada.
Aidha, walionyesha vitu vya dhihaka dhidi ya ibada ya Kiislamu, ikiwemo sanduku la katoni lililotengenezwa kuiga Kaaba. Khan alisema pia kuwa wanaume hao walileta nyama ya nguruwe (bacon) ili kuwachokoza na kuwalazimisha kuipokea.
Unyanyasaji ulizidi pale walipotoa maneno ya kibaguzi na shutuma zisizo na msingi dhidi ya wanafunzi wenye rangi. Khan alisema walihoji uraia wa wanafunzi na kutumia lugha ya matusi.
Mmoja alidai kuwa ni mwanajeshi mstaafu na kutoa vitisho. Baada ya sala, Khan alisema mmoja wao alijaribu kumrukia mwanafunzi.
Wanafunzi walisema hali kama hiyo haijawahi kutokea katika shughuli za MSA hapo awali. Khan alieleza tukio kuwa hilo limewaacha wakihisi kutokuwa salama katika sehemu ambayo awali walihisi kukaribishwa.
Hata hivyo, licha ya dhiki hiyo, wanafunzi walisema wataendelea kushikamana na maadili ya subira na heshima, wakifuata mfano wa imani yao.
Polisi wa USF wamethibitisha kuwa wanachunguza tukio hilo. Katika taarifa, chuo kikuu kimesema kinapitia video zinazozunguka mitandaoni na kitachukua hatua kwa mujibu wa sera za chuo na sheria za jimbo.
3495474