IQNA

Waislamu Marekani

Vita vya Gaza vyadumaza ushirikiano Waislamu na White House

21:03 - December 29, 2023
Habari ID: 3478109
IQNA - Baadhi ya viongozi wa Kiislamu wa Marekani wanaripotiwa kusita kufanya kazi na Ikulu ya White House katika kuandaa mkakati wa kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) kutokana na utawala wa Rais Joe Biden kuendelea kuunga mkono vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

 

Viongozi wa Kiisalmu ambao wamefanya kazi na utawala wa Biden hapo awali wana mashaka juu ya ufanisi wa mkakati huo na iwapo kweli White House ina nia safi katika kushirikiana na Waislamu..

Salam Al-Marayati, rais wa Baraza la Masuala ya Umma la Waislamu, ambaye pia ni mwanachama wa Muungano wa Jumuiya ya Waislamu wa Marekani, aliiambia CBS News kwamba yeye ni "ni vigumu sana hata kufikiria jinsi mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu utafanya kazi" wakati ambapo Waislamu wa Marekani wanahisi "hawako salama na hawaungwi mkono" wanaposhuhudia "mashambulio ya kutisha dhidi ya Wapalestina huko Gaza."

Alisema kuwa familia nyingi za Kiislamu, wanafunzi, na waajiriwa wanaogopa kuongea kuhusu jinai za Gaza kwa hofu ya kuadhibiwa, kwani baadhi ya watu ambao wamezungumza wamekabiliwa na "kupoteza kazi, kusimamishwa kazi, kudhibitiwa, kukadamizwa, uonevu na unyanyasaji wa makusudi."

Marekani imepiga kura ya turufu maazimio mawili ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kusitishwa kwa mapigano huko Gaza ambako mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7 yameua zaidi ya watu 21,500, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Marekani pia imetoa misaada ya kijeshi na kifedhakwa utawala wa Israel katika vita vyake dhidi ya Gaza.

Habari zinazohusiana
captcha