IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa

Uchochezi za NATO, Marekani umesababisha umeibua taharuki katika eneo

18:16 - February 25, 2022
Habari ID: 3474975
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehrah amesema, hatua za kichochezi zilizochukuliwa na shirika la kijeshi la NATO kwa uongozi wa Marekani zimetatanisha hali ya mambo katika eneo; na si hasha zikaifanya iwe tata zaidi.

Ayatullah Seyyid Ahmad Khatami ameashiria matukio ya Ukraine na operesheni maalumu ya kijeshi ya Russia ndani ya ardhi ya nchi hiyo na akasema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inazitolea mwito nchi zote zinazopigana kufanya mazungumzo na kuonyesha stahamala.

Mbali na kuashiria kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina wasiwasi wa kuuliwa watu wasio na hatia katika shambulio la kijeshi la Russia dhidi ya Ukraine, Ayatullah Khatami amesisitiza kuwa, hatua za kichochezi za NATO kwa uongozi wa Marekani zimetatanisha hali ya mambo katika eneo; na si hasha zikaifanya iwe tata zaidi.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amekumbusha kuhusu uingiliaji kijeshi wa Marekani katika maeneo mbalimbali ya dunia na akasema, katika shambulio la Russia dhidi ya Ukraine nchi za Ulaya zimekazania kupiga upatu wa vita na kila wakati zinachochea kuni kwenye moto wa vita hivyo, lakini msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ni wa pande mbili zinazopigana kuwa na stahamala na kuanza mazungumzo ya kuresha amani na utulivu.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khatami ameashiria pia mazungumzo ya Vienna na akasema: wawakilishi wa Iran katika mazungumzo ni watu wenye uchungu wa taifa lao na jitihada zao zote zinalenga kudhamini maslahi ya watu wetu na wanaelewa fika kwamba ghaya na lengo kuu ni kuondolewa vikwazo vyote; na kwa hivyo kama vikwazo havitaondolewa, mazungumzo hayatafikia mwafaka.

Katika hotuba yake ya kwanza, Khatibu wa Sala ya leo ya Ijumaa mjini Tehran amewausia waumini kuhusu uchamungu, subira katika maisha ya binafsi, muqawama katika njia ya haki, kujiimarisha zaidi kiimani katika kukabiliana na shubha na kushiriki katika masuala yote kwa basira na urazini kwa ajili ya kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu.

4038691

captcha