IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
21:52 - May 13, 2022
Habari ID: 3475244
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, safari za hivi karibuni ya Rais Bashar al-Assad wa Syria na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani nchini Iran zilikuwa za kimkakati na muhimu.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo leo katika ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran ambapo sambamba na kuashiria safari ya Rais wa Syria na kukutana kwake na Kiongozi Muadhamu amesema kuwa, safari hii imepelekea kuimarika zaidi kambi ya muqawama na Syria ipo mstari wa mbele wa muqawama na mapambano na utawala haramu wa Israel.

Aidha ameashiria safari ya jana ya Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani na mazungumzo yake na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kubainisha kwamba, safari hii licha ya kuwa ina umuhimu katika kupanua ushirikiano wa kiuchumi baina ya pande mbili, lakini lililo muhimu katika mazungumzo hayo ni matamshi ya Kiongozi Muadhamu ambaye alisema kuwa, Wazayuni kila wanapotia mguu hueneza ufisadi.

Khatibu wa muda Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesema pia kuwa, mataifa ya Ukanda wa Ghuba ya Uajemi yanapaswa kuwa na imani na Iran yenye nguvu kwani taifa hili ndilo ambalo litawasaidia haraka pale watakapokwama na kuhitajia msaada.

Ayatullah Khatami ameeleza bayana kwamba, Marekani, Uingereza na utawala wenye kutenda jinai wa Kizayuni wa Israel sio watu wa kutegemewa na kuegemewa, bali Iran ndio ya kutegemewa.

/4056651

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: