IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Port Said Misri kuanza Feb. 18

11:50 - February 05, 2022
Habari ID: 3474892
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Bandari ya Port Said Misri yamepangwa kuanza Februari 18.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo yatafunguliwa rasmi katika sherehe itakayohudhuriwa na Waziri Mkuu wa Misri Mustafa Madbouly.

Gavana wa Jimbo la Port Said Adel Mohamed Ibrahim Yousef Al Ghadhban anasema matayarisho yamekamilika na kwamba nchi 66 zitashiriki katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani.

Aidha amesema katika amshindano hayo mwanazuoni wa Kiislamu Ahmed Omar Hashem ataeneziwa pamoja na qarii maarufu wa Qur'ani Sheikh Ahmad Nuaina na mkuu wa Radio ya Qurani Misri Reda Abdel Salam.

Majaji katika mashindano hayo ni kutoka Misri, Imarati, Libya na Mali na watasimamiwa na Abdel Karim Saleh. Mashindano ya mwaka huu yamepewa jina la qarii Mustafa Ismail.

4033784

captcha