IQNA

Jinai za Israel

Walowezi wa Israel wamevamia Msikiti wa Al-Aqsa chini ya Ulinzi wa Kijeshi

12:24 - September 19, 2022
Habari ID: 3475808
TEHRAN (IQNA) -Walowezi wa Kizayuni wakiwa wanalindwa na askari wengi wa utawala haramu wa Israel walivamia uwanja wa Msikiti wa Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) siku ya Jumapili, na kufanya ibada za kichochezi za Kiyahudi katika eneo hilo takatifu la Kiislamu

Idara ya Wakfu ya Kiislamu inayomilikiwa na Jordan, inayosimamia eneo hilo takatifu, imesema kuwa, walowezi wengi Waisraeli waliingia ndani uwanja wa msikiti huo kupitia lango la Morocco (Bab al-Maghariba) kwa makundi na kufanya ibada za  Talmudi hapo chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi wa Israel.

Hayo yanajiri huku kukiwa na wito wa mashirika ya mrengo wa kulia ya Kizayuni yakiwa yanawatala Waazyuni kuingia katika eneo hilo takatifu la Kiislamu kwa wingi mnamo Septemba 29 katika hafla ya Mwaka Mpya wa Kiyahudi.

Tangu mwaka wa 2003, utawala vamizi wa Israel umekuwa ukiwaruhusu walowezi wa Kizayuni kuingia ndani ya Msikiti wa Al Aqsa kila siku, isipokuwa Ijumaa, siku ya sala ya kila siku ya Ijumaa ya Waislamu.

Wakfu wa Kiislamu mara kwa mara umekuwa ukieleza kuwepo kwa Walowezi hao katika Msikiti wa Al-Aqsa kuwa ni wa uchochezi na kusema kuwa, waumini wa Kipalestina na walinzi wa Al-Aqsa wanalaani vikali uwepo wa Wazayuni katika eneo hilo takatifu la Kiislamu.

Utawala dhalimu wa Israel ulikalia Quds Mashariki , ulipo Msikiti wa Al-Aqsa, wakati wa Vita vya Siku Sita mwaka 1967 katika hatua ambayo haijawahi kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

3480529

captcha