IQNA

Jinai za Israel

Indhari ya chama kikubwa zaidi Jordan kuhusu ongezeko la Walowezi Kizayuni huko Al-Aqsa

22:49 - September 22, 2022
Habari ID: 3475824
TEHRAN (IQNA) - Chama kikubwa zaidi nchini Jordan kimeonya kuhusu ongezeko la walowezi wa Kizayuni Waisraeli ambao wanatekeleza hujuma za kichochezi dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa huko al-Quds (Jerusalem).

Chama cha The Islamic Action Front kimesema katika taarifa iliyotolewa na kamati yake ya al-Quds na Palestina, kwamba ongezeko linalotarajiwa la hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa wakati wa msimu wa sikukuu za Kiyahudi ni "shambulio la wazi dhidi ya utakatifu wa msikiti huo, uchochezi kwa Waarabu na Waislamu mbali na kuwa ni hujuma  dhidi ya  mamlaka ya Jordani juu ya maeneo matakatifu."

Kikikemea kitendo cha jeshi la Israel cha kumkamataa na kumuweka kizuizini hivi Mkurugenzi wa Msikiti wa Al-Aqsa, Omar Al-Kiswani, chama hicho pia kimelaani kuendelea kwa sera ya Israel ya kuwafukuza wafanyakazi na waumini katika msikiti huo, ambao wanakabiliana na walowezi  wa Kizayuni na miradi yao inayolenga kuigawanya Al-Aqsa.

Chama hicho kiliwataka wananchi wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Al  Quds na ardhi  zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina la Israel "kujikusanya kuelekea Msikiti wa Al-Aqsa, na kukabiliana na walowezi hao". Aidha chama hicho kikubwa cha kisiasa nchini Jordan kimewataka raia mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za kivitendo za kuunga mkono Al-Aqsa, na kuzishinikiza serikali zao kubeba wajibu wao wa kukabiliana na "mashambulizi ya Wazayuni".

Jordan pia inapaswa "kuchukua majukumu yake kufuatia shambulio dhidi ya  walinzi wa Jordan wa Msikiti wa Al-Aqsa, na kuchukua hatua madhubuti na imara za kukomesha kuongezeka kwa Wazayuni katika maeneo matakatifu ya Kiislamu huo Palestina, na sio kujitosheleza kwa taarifa za kulaani," iliongeza.

Likizo za Kiyahudi za Rosh Hashanah - Mwaka Mpya - na Yom Kippur zinafanyika katika wiki zijazo Wazayuni Mayahudi wa mrengo wa kulia wakijiandaa  kuvamia Msikiti wa Al-Aqsa kwa wingi.

3480591

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha