IQNA

Jinai za Israel

Wapalestina 20 wajeruhiwa katika mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni mjini Quds

23:35 - September 21, 2022
Habari ID: 3475819
TEHRAN (IQNA) – Walowezi wa Kizayuni waliwashambulia Wapalestina katika Mji Mkongwe wa al-Quds (Jerusalem) na kujeruhi takriban 21 kati yao wakiwemo watoto.

Vyanzo vya habari vilisema kuwa watoto na wazee walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa wakati waliposhambuliwa na Wazayuni wakiwa sokoni katika jiji la kalela  al Quds.

Mmiliki wa duka Sami Salhab alisema kuwa mashambulizi kama hayo hutokea chini ya ulinzi wa majeshi ya Israel karibu kila siku.

Alisema walowezi hao walivamia soko hilo na kuvamia kundi la wafanyakazi walipokuwa wakifanya matengenezo katika moja ya maduka hayo.

Walowezi hao wa Kizayuni watenda jinai waliwapulizia gesi ya pilipili Wapalestina katika soko hilo, wakiwemo watoto.

Wakati huo huo, Wayahudi 255 wa Israel wenye itikadi kali walivamia Msikiti wa Al-Aqsa hapo jana na kufanya ibada za kichochezi za Talmud.

Mashambulio ya walowezi na uvamizi wa Al-Aqsa yanatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo huku Wayahudi wakisherehekea Rosh Hashanah - Mwaka Mpya wa Kiyahudi - na Yom Kippur.

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha