IQNA

Waislamu Kanada

Hujuma dhidi ya Msikiti wa Toronto ni ishara ya ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu

18:48 - October 21, 2022
Habari ID: 3475963
TEHRAN (IQNA) – Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Kanada (NCCM) limeashiria kisa cha hujuma dhidi ya msikiti wa eneo la Toronto kama ishara ya "kuongezeka kwa kutisha kwa chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia)".

Hujuma hiyo iliyofanyika wiki iliyopita katika Kituo cha Kiislamu cha Imam Mahdi (AS) huko Thornhill ilikuwa kwa sura ya maandishi yenye msukumo wa chuki yaliyoandikwa kwa Kiajemi. Msikiti huo pia umepokea vitisho vya mabomu na waumini wametishiwa kwa mujibu wa NCCM.

Lakini ni moja tu ya mamia ya mifano ya matukio ya chuki dhidi ya Uislamu kote Kanada (Canada).

"Jumuiya ya Waislamu nchini Kanada imeathiriwa na zaidi ya jumbe 1,000 za chuki dhidi ya Uislamu kwenye Twitter pekee katika siku chache zilizopita," NCCM iliandika Alhamisi kwenye Facebook. "Hizi ni pamoja na vitisho vya kuuawa, vitisho vya vurugu, na unyanyasaji wa mara kwa mara. Inatosha. Hii lazima ikome."

Kundi hilo lilifanya mkutano na waandishi wa habari Alhamisi "kushughulikia uharibifu wa hivi karibuni uliochochewa na chuki dhidi ya Uislamu na vitisho vilivyoelekezwa kwa jamii" na kuwataka maafisa kusaidia kudhibiti chuki inayoelekezwa kwa Waislamu wa Kanada.

Polisi wana picha ya mwandishi wa maandishi ya kichochezi ambayo ilinaswa kwenye kamera ya usalama na wametoa maelezo ya mshukiwa. Mamlaka ilitoa wito kwa wananchi kujitokeza na taarifa kuhusiana na tukio hilo.

3480932

captcha