IQNA

Waislamu Kanada

Waislamu katika Okotok nchini Kanada Hatimaye Wamepata Mahali pa Sala ya Ijumaa

21:10 - December 27, 2022
Habari ID: 3476316
TEHRAN (IQNA) – Waislamu katika mji wa Okotoks nchini Kanada sasa wana nafasi ya Sala ya Ijumaa kufuatia ushirikiano na kanisa moja la mji huo.

Waislamu katika jiji hilo hapo awali walilazimika kusafiri kwenda mbali sana kwa ajili ya  sala ya Ijumaa ambapo baadhi walienda katika mji wa  Calgary au hadi High River.

Sasa jumuiya ya Waislamu imeshirikiana na Kanisa la Okotoks United Church, ambalo limekubali kukodisha jumuiya mahali pa sala kila Ijumaa.

Inamaanisha kuwa jamii ya Kiislamu inayozidi kuongezeka sasa ina mahali pa  kukutanikia ambayo imekosekana kwa miaka mingi.

"Ilikuwa muhimu sana kwangu nilipohamia hapa miezi sita iliyopita kutoka Toronto. Hilo ni jambo moja ambalo nilikuwa nikikosa," Salam Akhtar alisema.

"Sasa kwa kuungwa mkono na jumuiya yetu kubwa huko Calgary, tuliweza kuanzisha harakati hii, na ni hatua ya kwanza tu lakini yenye umuhimu mkubwa," alisema Akhtar.

Kwa wengine inamaanisha kuwa muda wa kutokuwa kazini Ijumaa  sasa utapungua.

"Nilikuwa nikienda kusali High River," alisema Mohamed Desouki, anayeishi Calgary lakini anafanya kazi Okotoks.

"Nililazimika kuondoka kazini kwa saa moja na nusu na sasa eneo la kusali ni dakika mbili tu kutoka kazini. Ni rahisi zaidi," Desouki alisema.

Mjomba wa Desouki aliwasili Alberta mnamo 1905 na alihusika katika ujenzi wa msikiti wa kwanza huko Calgary.

Imam wa Calgary Syed Soharwardy alifunga safari hadi Okotoks ili kuandaa sala ya kwanza ya kihistoria ya Ijumaa hapo, na ameitaja sala hiyo kuwa tukio la kihistoria kwa jumuiya yao.

Takriban watu 30 walijitokeza kwa ajili ya Sala ya  kwanza ya Ijumaa mapema mwezi huu.

3481845

Kishikizo: okotoks kanada waislamu
captcha