IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Machafuko bila shaka yatakomeshwa na taifa la Iran litaendelea kusonga mbele

17:04 - November 19, 2022
Habari ID: 3476116
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema lengo kuu la wachochezi wa machafuko ya hivi karibuni ni kuliingiza taifa la Iran katika medani na kuongeza kuwa: "Machafuko hayo bila shaka yatakomeshwa na taifa kuendelea kusonga mbele kwa nguvu zaidi na ari mpya katika uwanja wa maendeleo ya nchi."

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu, Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo Jumamosi mjini Tehran katika kikao na watu wa mkoa Isfahan na kuongeza kuwa: "Matukio haya, jinai na uharibifu huu unaleta matatizo kwa watu na wafanyabiashara, lakini walio mstari wa mbele na nyuma ya pazia ya shari na maovu haya ni watu duni sana na hivyo hawawezi kuudhuru mfumo (wa Kiislamu)."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amesema: "Tatizo kubwa la uistikbari kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ni kwamba iwapo mfumo huu utaendelea na kuonekana duniani, basi mantiki ya demokrasia ya kiliberali katika ulimwengu wa Magharibi itabatilika."

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: "Kwa sababu ya hasira na ghadhabu hiyo, watawala wa Marekani na Ulaya wanaingia uwanjani kwa njia zote zinazowezekana, lakini hawawezi kufanya lolote lenye madhara, kwani hawakuweza kulifanya hilo hapo awali na pia hawataweza kulifanya katika siku zijazo."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameashiria ujanja wa Wamagharibi wanavyotumia jina la uhuru na demokrasia dhidi ya uhuru na demokrasia katika nchi zingine na kuongeza kuwa: "Nchi ya Afghanistan ni mfano wa karibu na wa wazi ambapo Wamarekani walifanya shambulio la kijeshi katika nchi hiyo chini ya kisingizio cha serikali kutokuwa ya wananchi lakini baada ya miaka 20 ya uhalifu na uporaji, serikali hiyo hiyo waliyotangaza kuwa wanataka kuiondoa imerejea madarakani huku Wamarekani wakiondoka kwa fedheha".

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amebainisha kuwa katika makabiliano ya kimsingi ya Iran na madola ya kiistikbari, Marekani iko mstari wa mbele na Ulaya iko nyuma ya Marekani, na akaongeza kuwa: Katika miaka ya baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, marais wote wa Marekani wakiwemo Wademocrat  Carter, Clinton, na Obama na hali kadhalika Warepublican Reagan na Bush kama mbwa wenye kichaa hadi Rais wa sasa ambaye hana fahamu, wanadai wanataka kulikomboa taifa la Iran. Wote wamesimama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wamekuwa wakiomba msaada wa kila aliye na uwezo kuwasaidia ukiwemo utawala wa Kizayuni kama mbwa wao aliyefungwa nyororo na pia baadhi ya nchi za eneo.

Ayatullah Khamenei amesema uwezo wa  kutumia fursa ya vitisho ni dhati ya asili ya taifa lenye  imani na kuongeza: Historia ya wananchi wa Iran katika kuibua fursa kuanzia zama za kujihami kutakatifu hadi leo kumewafanya maadui watambue kuwa, kila wanapotaka kutumia nguvu za kijeshi taifa la Iran haliwezi kushindwa hata kidogo. Taifa la Iran limewafahamisha Wamarekani na wapinzani kuwa, "Kufika kwenu hapa ni uamuzi wenu, lakini si kuondoka kwenu," na kwamba "iwapo mtafanya hujuma ya kichokozi, mtakamatwa na kuangamizwa."

4100642

captcha