IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mshindi wa Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu

19:27 - November 23, 2022
Habari ID: 3476136
TEHRAN (IQNA) – Ahmed Kuzu kutoka Uturuki aliibuka mshindi katika Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Kusoma Qur'ani ya Moscow, nchini Russia

Hii hapa klipu ya qiraa yake.

Mashindano ya 20 Kimataifa ya Kusoma Qur'ani ya Moscow yalikamilika katika hafla ya Jumapili usiku katika mji huo mkuu wa Urusi (Russia), ambapo walioshika nafasi za tatu za juu walitangazwa na kutunukiwa zawadi.

Kulingana na tangazo la jopo la majaji, mwakilishi wa Uturuki Ahmed Kuzu aliibuka mshindi katika mashindano hayo

Mshindi wa pili alikuwa Abdul Rahman Faraj kutoka Misri na qari wa Iran Seyed Mostafa Hosseini aliibuka wa tatu.

Nafasi ya nne iilikwenda kwa qari aliyewakilisha Yemen.

Wasomaji wa Qur'ani kutoka nchi 21 zikiwemo Russia, Bahrain, Sudan, Umoja wa Falme za Kiarabu, Syria, Morocco, Tajikistan, Kazakhstan, Tanzania na Bangladesh walishiriki katika hafla ya kimataifa ya Qur'ani iliyoanza Ijumaa mjini Moscow.

Baraza la Mufti la Russia liliandaa hafla hiyo kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu..

Wajumbe wa jopo la majaji walikuwa wataalamu wa Qur'ani kutoka Yemen, Uturuki, Lebanon, Russia, na Saudi Arabia.

4101491

captcha