IQNA

Mashindano ya 22 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Moscow kuwa na wawakilishi wa nchi 30

16:53 - October 19, 2024
Habari ID: 3479617
IQNA - Mashindano ya 22 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Moscow yatafanyika katika mji mkuu wa Russia mwezi ujao.

Mashindano hayo yameandaliwa na Utawala wa Kiroho wa Waislamu wa Shirikisho la Urusi,  na yatafanyika huko Moscow kutoka Novemba 6 hadi 8.

Wasomaji wakuu wa Qur'ani kutoka zaidi ya nchi 30 watashiriki katika mashindano hayo. Washiriki wataonyesha ujuzi na umahiri wao katika kusoma Qur'ani Tukufu.

Mashindano hayo yatafanyika katika Msikiti wa Jamia wa Moscow.

Sherehe za kufunga mashindano hayo zinatarajiwa kufanyika Novemba 8. Mbali na mashindano ya Qur'ani kutakkuwa pia na tamthili ya "Dafina za Qur'ani", kuhusu maana za kina za aya za Qur'an Tukufu.

3490336

Habari zinazohusiana
captcha