IQNA

Watetezi wa Palestina

Kongamano la 19 la Kimataifa la Waislamu la Russia lajadili hali ya Gaza

22:09 - December 13, 2023
Habari ID: 3478028
IQNA – Toleo la 19 la Jukwaa la Kimataifa la Russia na Ulimwengu wa Kiislamu lilifanyika mjini Moscow huku wazungumzaji wakizingatia hali mbaya ya Gaza.

Viongozi wa kidini, mabalozi na maafisa wa kisiasa kutoka nchi 18 walihudhuria mkutano huo uliofanyika katika Msikiti wa Jamia wa Moscow siku ya Jumanne.

Akihutubia katika hafla hiyo, Sheikh Ravil Gainutdin, Mwenyekiti wa Baraza la Kiroho la Waislamu wa Shirikisho la Russia na Baraza la Mufti wa Russia alisema kuwa, kuanzishwa kwa taifa la Palestina kunashikilia ufunguo wa kukomesha vita na kustawisha amani na utulivu wa kudumu katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Sheikh Gainutdin alijadili kwa kina hali  ya Palestina, akizungumzia asili ya ardhi hiyo kihistoria na mzozo wa muda mrefu wa miaka 76 ambao umesababisha kupoteza maisha ya watu 100,000 na watu milioni kadhaa kuyahama makazi yao.

Ameashiria hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, ambapo vita vya mauaji ya kimbari vya utawala haramu wa Israel tangu Oktoba 7 vimesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina karibu 19,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Akisisitiza umuhimu wa suluhisho la kisiasa, Sheikh Gainutdin alionya kuhusu  kuendeleza vita, akionya kwamba inaweza kuchochea migogoro zaidi.

Aidha alisisitiza msimamo wa Russia wa kuunga mkono kuanzishwa taifa huru la Palestina ndani ya mipaka ya mwaka 1967, mji mkuu wake ukiwa Mashariki mwa al-Quds.

Hujjatul Islam Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, alisisitiza uadilifu kama tunu kuu ya kijamii, akisisitiza umuhimu mkubwa wa suala la Palestina kama kipaumbele cha juu cha ulimwengu wa Kiislamu.

Naye Kazem Jalali, Balozi wa Iran mjini Moscow, alilaani ukatili wa utawala wa Israel ambao uwepo wake kwa miongo saba ni doa chafu kwa ubinadamu.

Abdel Hafiz Nofal, Balozi wa Palestina mjini Moscow, alitafakari kuhusu miaka 75 ya utawala wa Israel katika ardhi ya Wapalestina, akisisitiza azma isiyoyumba ya kila Mpalestina kusalia katika ardhi yao licha 

Habari zinazohusiana
captcha