TEHRAN (IQNA)- Mwanamasumbwi wa kulipwa wa zamani wa Marekani, Mike Tyson, amefika katika mji mtakatifu wa Makka, eneo takatifu zaidi katika Uislamu, na kutekeleza ibada ya Umrah (Hija Ndogo).

Ameandamana katika safari hiyo na mwanamuziki Mmarekani, DJ Khalid ambaye amesambaza klipu za video wakiwa katika Ka'aba Tukuf mjini Makka.
Ameandika katika mitando ya kijamii kuwa: "Nilipoingia Makka nilitokwa na machozi ya furaha. Katika maisha yangu yote nimekuwa na hamu sana na kufika na kusali katika Msikiti Mtakatifu wa Makka na kumshukuru Allah. Nimeomba kuwe na mahaba zaidi duniani na ipatikane amani, furaha, afya na salama kwa wote."
Ikumbuwke kuwa Mike Tyson alisilimu na kuukubali Uislamu kama imani yake mwaka 1992.
3481613