"Hatuwezi kuendeleza kundi hilo la Wanawake wa Kiislamu kwa ajili ya Harris-Walz, kwa sababu timu ya Hariss ilikataa ombi lao la kutaka msemaji wa Kipalestina achukue jukwaa kwenye DNC," kikundi hicho kimesema.
Mazungumzo katika kongamano hilo yalikuwa yakiendelea kwa wiki nzima. Hata hivyo, katika saa za mapema za Alhamisi asubuhi, siku ya mwisho ya kongamano hilo, Abbas Alawieh, wanaharakati watetezi wa Palestina walifahamishwa kwamba hakuna Mpalestina atakayeruhusiwa kuzungumza wakati wa hafla hiyo.
Akizungumza katika kipindi cha "The Ray Hanania Radio Show" wiki hii, Nasser Beydoun, Mmarekani wa Lebanon, alisema Wamarekani Waarabu na Waislamu wanataka kumuunga mkono Harris lakini hawawezi kujitolea hadi atoe kauli "ya wazi " inayounga mkono kuundwa kwa taifa la Palestina. , pamoja na kukomesha mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza."
Kwa uungaji mkono kamili wa kisiasa na kijeshi kutoka kwa Utawala wa Joe Biden, utawala wa Israel ulianzisha vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa mwezi Oktoba mwaka jana. Uvamizi huo wa Israel umepelekea kuuawa shahidi Wapalestina zaidi ya 40,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Mashambulizi hayo pia yamewafanya takriban wakazi wote milioni 2.3 wa Gaza kuwa wakimbizi huku kukkiwa uhaba wa chakula, maji na dawa.
3489615