Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, tukio hilo lilitokea mwendo wa saa 5:40 usiku. katika Jumuiya ya Kiislamu ya Gastonia, iliyoko katika mtaa wa 4000 wa Barabara ya Titman.
Uharibifu wa madirisha matatu unakadiriwa kusababisha hasara ya dola 900. Nathan Reynolds Webster, 32, alikamatwa na kushtakiwa kwa uharibifu wa mali.
Tovuti ya Ofisi ya Polisi ya Gaston inaonyesha kuwa aliachiliwa muda mfupi baada ya kufungwa jela, akiwa na dhamana ya dola 1,000. Uharibifu huo unakuja huku kukiwa na ongezeko la uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani, hasa tangu Oktoba mwaka jana wakati utawala wa Israel ulipanzisha mauaji ya kimbari dhidi ya Palestina.
3489220