IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu / 32

Msingi wa Umoja wa Kiislamu wa Tarjuma ya Qur'ani ya Kijapani ya Tatsuoichi Savada

21:57 - November 14, 2023
Habari ID: 3477892
TEHRAN (IQNA) - Tafsiri au tarjuma ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kijapani ya Tatsuoichi Savada ilichapishwa mnamo 2014.

Katika tafsiri hii, Savada amejaribu kuzingatia umoja wa Kiislamu na pia kuziba mapengo ya kitamaduni na kisarufi kati ya lugha za Kiarabu na Kijapani.

Tafsiri kamili ya kwanza ya Qur'ani Tukufu kwa Kijapani ilitolewa mwaka wa 1920 na kufikia mwaka wa 2015, idadi ya tafsiri za Qur'ani za Kijapani ilifikia 14, 10 kati ya hizo zilijumuisha aya zote za Qur'ani Tukufu.

Savada alitayarisha tafsiri hiyo, ambayo ilichapishwa mwaka wa 2014, kwa mtazamo wa Shia na kufaidika na baadhi ya wafafanuzi wa Kurani kama vile Al-Mizan na Nemouneh pamoja na tafsiri za Kiajemi za Qur'ani ili kuimarisha kazi yake.

Savada amejaribu kuweka umoja wa Kiislamu kuwa msingi wa kazi yake na kutafsiri aya za Qur'ani Tukufu kwa kuzingatia mtazamo wa kukuza umoja na kuepusha mifarakano ya kimadhehebu.

Tafsiri yake imeondoa baadhi ya matatizo yaliyokuwepo katika tafsiri zilizopita, zikiwemo zile zinazotokana na ukosefu wa baadhi ya dhana kama vile ufufuo katika utamaduni wa Kijapani na pia tofauti za sarufi za Kiarabu na Kijapani.

Savada alizaliwa Tokyo mwaka 1964. Ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa nchini Iran katika fani ya mafundisho ya Kiislamu.

Kwa sasa anahudumu kama naibu wa tawi la chuo kikuu hicho nchini Japani na anafundisha huko pia.

Baadhi ya kazi zake zilizochapishwa ni pamoja na:

- Tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwa Kijapani

- Tafsiri ya kitabu "Jinsi ya Kusali"

- Tafsiri na mkusanyiko wa kamusi ya maneno ya Qur'ani Tukufu

- Mhariri wa tafsiri ya Kijapani ya mfululizo wa mihadhara ya Ayatullah Makarem Shirazi kuhusu imani za Kiislamu

- Mhariri wa tafsiri ya Kijapani ya mfululizo wa mihadhara ya Ayatullah Mosuavi Lari kuhusu imani za Kiislamu

- Mhariri wa tafsiri ya Kijapani ya kitabu 'Irfani ya Kiisalmu' cha Ustadh Murtadha Motahhari)

- Mhariri wa tafsiri ya Kijapani ya kitabu Usul al Kafi

- Mhariri wa tafsiri ya Kijapani ya barua ya Imam Ali (AS) kwa Malik Ashtar

Kishikizo: Wanazuoni Mashuhuri
captcha