IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu 30

Tofauti katika Tarjuma za Kifaransa za Qur'ani Tukufu

20:36 - September 30, 2023
Habari ID: 3477672
TEHRAN (IQNA) – Kuna zaidi ya tarjuma au tafsiri 120 za Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa, ambazo baadhi yake zina sifa zake maalum na nyingine zimefasiriwa kwa kuiga zile zilizotangulia huku kukiwa na mabadiliko machache sana.

Mukhtar Zawawi, profesa wa isimu na lugha ya Kifaransa katika Kitivo cha Fasihi, Lugha na Sanaa cha Chuo Kikuu cha Djillali Liabes Sidi Bel Abbes nchini Algeria, wameandika vitabu viwili vinavyojadili tarjuma za Kifaransa za Qur'ani Tukufu

Kitabu chake cha kwanza juu ya mada hii kinaitwa "Semiotics of Translation of the Text of Quran", ambacho kilichapishwa mnamo 2015.

Aliandika kitabu cha pili chini ya kichwa cha " Chapters in Pragmatics of Quran Translation " ambacho kilichapishwa mnamo 2018.

Zawawi pia ameandika makala kadhaa juu ya mada hii.

Anasema kilichomfanya apende kusoma tafsiri za Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa ni idadi kubwa ya tarjuma, ambazo ni zaidi ya 120. Amekusanya na kusoma zaidi ya 50 kati ya hizo.

Kwa mujibu wa Zawawi, kuwepo kwa tafsiri mbalimbali za Qur'ani Tukufu katika lugha ya Kifaransa kuna sababu tofauti, baadhi zikiwa zinahusiana na mfasiri huku nyingine zikitokana na umahiri wa lugha ya Kifaransa.

Pia kuna tofauti ambazo zinatokana na tarjuma au tafsiri tofauti za maandishi ya Qur'ani Tukufu, anabainisha.

Mwanazuoni huyo wa Algeria anasema katika vitabu vyake viwili pamoja na makala zinazohusu suala hilo ametoa mwanga kuhusu sababu ya kuwepo tofauti nyingi katika tafsiri zilizopo za Qur'ani kwa lugha ya Kifaransa.

Kishikizo: Wanazuoni Mashuhuri
captcha