IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /57

Hatua katika Maisha ya Mwanadamu Kwa mujibu wa Sura Al-Hadid

18:47 - January 16, 2023
Habari ID: 3476411
TEHRAN (IQNA) - Kuna hatua tofauti katika maisha ya mtu ambayo kila moja ina sifa zake kutokana na umri na masharti ya mtu. Kwa mujibu wa Sura Al-Hadid ya Qur'ani Tukufu, maisha ya mwanadamu yana hatua tano.

Al-Hadid ni sura ya 57 ya Qur'ani Tukufu yenye aya 29 na ipo katika Juzuu ya 27. Ni Madani na ni Sura ya 94 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina la Sura linatokana na neno Hadid, ambalo maana yake ni chuma, na neno hilo liko katika aya ya 25.

Tauhidi, sifa za Mwenyezi Mungu, adhama ya Qur'ani Tukufu, na hali za waumini na makafiri Siku ya Kiyama ni miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika Sura hii.

Pia inazungumzia kuhusu uumbaji katika siku sita na vilevile hadithi za baadhi ya manabii kama Nuhu (AS) na Ibrahim (AS) na jinsi Yesu au Issa (AS) alivyofikia utume na jinsi Biblia ilivyoteremshwa.

Aya za kuanzia zinahusu imani ya Mungu mmoja na sifa za Mwenyezi Mungu, zikiorodhesha baadhi ya sifa 20 za Mwenyezi Mungu.

Kisha inasema Mwenyezi Mungu anaufanya usiku kuingia katika mchana na mchana kuingia katika usiku na jinsi urefu wa mchana na usiku unavyobadilika katika majira mbalimbali, jambo ambalo linaonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu na utawala wake duniani na mbinguni.

Adhama ya Qur'ani na sifa zake, hali ya makundi mawili ya waumini na makafiri Siku ya Kiyama na hatima ya watu walioishi kabla na hawakumuamini Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa katika Sura Al-Hadid.

Sura inagawanya maisha ya mwanadamu katika hatua tano: kucheza, kujifurahisha, kujipamba, kujifakharisha, na kushindana kwa utajiri mkubwa na watoto. Vipengele hivi vinaendana na hatua za maisha katika umri tofauti.

Sehemu kubwa ya Sura ni kuhusu kuwa mkarimu katika njia ya Mwenyezi Mungu na jinsi mali za kidunia zisivyo na thamani. Pia inarejelea kuzingatia uadilifu katika kijamii kama lengo kuu la wajumbe wa Mungu.

Surah Al-Hadid inakosoa utengano wa kijamii na utawa na inasema Mwenyezi Mungu hakuagiza hayo.

captcha