IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 55

Sura Ar-Rahman; Swali la Mwenyezi Mungu kuhusu kukanusha Neema

20:54 - January 11, 2023
Habari ID: 3476385
TEHRAN (IQNA) – Mwenyezi Mungu amewapa wanadamu neema nyingi lakini watu hawamthamini Muumba kiukweli au wanafikiria kimakosa kwamba Mwenyezi Mungu hawazingatii vya kutosha.

Al-Rahman ni sura ya 55 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 78 na iko katika Juzuu ya 27. Wanachuoni wametoa mitazamo tofauti kuhusu iwapo ni Makki au Madani. Ar-Rahman ni Sura ya 97 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Inajulikana kama Bibi-Arusi wa Qur'ani Tukufu, kulingana na Hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina la Sura linatokana na neno Ar-Rahman (Mwingi wa Rehema), ambalo ni sifa ya Mwenyezi Mungu, na liko katika Aya ya kwanza.

Sura inauchukulia ulimwengu kuwa unafuata amri ambayo wanadamu na majini wananufaika nayo. Inagawanya ulimwengu katika makundi mawili: ya muda mfupi wa mpito na ya kudumu.

Inasema kwamba katika akhera, furaha na huzuni, malipo na adhabu vinatenganishwa.

Sura inasisitiza kwamba ulimwengu wote, yaani  ulimwengu huu na ujao, una mfumo uliounganishwa na kwamba chochote kilichopo duniani ni neema ya Mwenyezi Mungu. Ndio maana inawauliza wanadamu na majini mara 31: Ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?

Sura inaanza na rehema za Mwenyezi Mungu zinazovifunika viumbe vyote na kuishia kwa kumsifu Mola.

Surah Ar-Rahman inataja neema za Mwenyezi Mungu hapa duniani na Akhera. Pia inazungumzia Siku ya Kiyama na sifa zake na jinsi matendo ya watu yanakadiriwa.

Katika sura hii, mafundisho ya Qur'ani Tukufu, uumbaji wa mwanadamu na majini, uumbaji wa mimea, miti, na mbingu, utawala wa sheria, uumbaji wa ardhi na sifa zake, uumbaji wa matunda, maua na mboga, na kuunganisha bahari mbili ( ya maji ya chumvi maji na ya maji matamu) yametajwa kuwa ni baadhi ya fadhila za Mungu.

Aya ndogo kabisa ya Quran pia imo katika Sura hii: “Za kijani kibivu.” (aya ya 64)

Katika aya ya 19 na 20, inazungumzia juu ya bahari mbili: “Anaziendesha bahari mbili zikutane. Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.”

Wasomi wanaamini kizuizi kilichoashiriwa hapo ni kile cha Bahari ya Adriatic na Bahari ya Kaskazini karibu na Denmark.

captcha