IQNA

Mashindano ya Qur'ani Nigeria

Washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani nchini Nigeria watunukiwa

18:08 - January 23, 2023
Habari ID: 3476450
TEHRAN (IQNA) - Washindi wakuu wa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu nchini Nigeria walitunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika Sokoto.

Gavana wa Jimbo la Sokoto, Aminu Tambuwal, ametoa zawadi ya Naira  milioni 10 kwa Nur Abdullahi, ambaye aliibuka mshindi wa jumla wa Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur’ani.

Sultani wa Sokoto, Abubakar Sa’ad, pia alimtukuza mshindi kwa taji la jadi la Modibbon Sokoto.

Hafla ya kuwatunuku washindi ilifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kasarawa huko Sokoto siku ya Jumapili. Mashindano hayo lilifanyika hivi karibuni huko Gusau, Jimbo la Zamfara.

Mshindi, mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kompyuta, kutoka Jimbo la Sokoto, alikuwa mzaliwa wa kwanza wa jimbo hilo kushinda shindano la kila mwaka tangu kuanzishwa kwake mnamo 1986.

Serikali ilimtunuku Abdullahi nafasi ya kazi katika Huduma ya Kiraia ya Sokoto, udhamini wa masomo ya Uzamili na Uzamivu na nafasinne za Hija, msaidizi wa vyombo vya habari wa gavana, Muhammad Bello, alisema.

Gavana huyo pia alimtunuku Zainab Mahmoud, ambaye alishinda shindano la wanawake, zawadi ya pesa taslimu Naira milioni 3 na kiti cha hajj.

Sultani wa Sokoto alitoa pesa taslimu Naira nusu miliono kwa niaba ya Baraza la Kisultani, kwa Bi Mahmoud.

3482180

captcha