IQNA

Jinai za Israel

Meya wa Barcelona avunja uhusiano na Tel Aviv kuhusu ubaguzi wa rangi wa Israel

17:57 - February 10, 2023
Habari ID: 3476542
TEHRAN (IQNA) - Meya wa jiji la Uhispania la Barcelona ametangaza kusimamisha uhusiano na Tel Aviv kutokana na Israel kukiuka haki za watu wa Palestina kwa njia "iliyoratibiwa".

Ada Colau alitangaza uamuzi huo katika barua kwa Waziri Mkuu wa utawala haramu Israel Benjamin Netanyahu. Alisisitiza kuwa jiji hilo litasitisha uhusiano hadi Israeli itakapoacha "ukiukaji ulioratibiwa  wa haki za binadamu wa Palestina."

"Nimeamua kusimamisha kwa muda uhusiano na Israel na taasisi rasmi za huko - ikiwa ni pamoja na makubaliano ya pande mbili na Halmashauri ya Jiji la Tel Aviv - hadi mamlaka ya Israeli itakapokomesha mfumo wa ukiukaji haki za watu wa Palestina na kuzingatia kikamilifu majukumu yake kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa. Hatuwezi kukaa kimya," aliandika.

Kwa mujibu wa meya huyo, uamuzi huo ulitolewa baada ya makundi 100 na wakazi zaidi ya 4,000 kutia saini ombi la kuvunja uhusiano na utawala unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Wizara ya mambo ya nje ya Palestina ilikaribisha uamuzi wa Barcelona, ​​ikitoa wito kwa miji mingine kuiga mfano huo na kuchukua hatua sawia.

Imebainisha kuwa, hatua hizo zitauwekea mashinikizo utawala ghasibu wa Israel uache ukiukaji na jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina, ardhi zao na matakatifu yao, na kukomesha hatua zake zote haramu za upande mmoja zinazodhoofisha fursa za amani.

Utawala wa Israel umewaua maelefu ya Wapalestina wanaopinga kukaliwa kwa ardhi zao na utawala huo ghasibu tangu vita vya mwaka 1967.

Mwezi Januari pekee, wanajeshi wa Israel waliuwa Wapalestina  zaidi ya 42 wakiwemo watoto 8, huku Wapalestina 224, wakiwemo watoto 61, wakiuawa katika hujuma za wanajeshi katili wa Israel mwaka 2022.

Utawala wa Israel unawapa hadhi maalum walowezi haramu wa Kizayuni huku  Wapalestina wakiwa  hawana haki na ulinzi sawa wa kisheria. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesisitiza kuwa Israel inatekeleza jinai ya kimataifa ya ubaguzi wa rangi kwa kukiuka haki za Wapalestina.

captcha