IQNA

Jinai za Israel

Jeshi katili la Israel laua Wapalestina 9 katika jinai ya kinyama mjini Jenin

21:11 - January 26, 2023
Habari ID: 3476467
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamevamia kambi ya wakimbizi wa Palestina katika mji wa Jenin na kuwauwa shahidi Wapalestina 9.

Katika siku, wiki na miezi ya hivi karibuni wanajeshi wa utawala wa kizayuni wameshadisha mashambulizi dhidi ya raia wa Palestina katika maeneo mbalimbali ya ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel khususan katika mji wa Jenin. Wanajeshi wa utawala  ghasibu unaoikalia Quds kwa mabavu mara kwa mara wamekuwa wakiwalenga kwa risasi za moja kwa moja raia wa Palestina.    

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamevamia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina huko Jenin na kuwauwa shahidi Wapalestina 9 akiwemo bibi kizee mmoja. Wapalestina wasiopungua 16 pia wamejeruhiwa katika hujuma hiyo ya kikatili ya Wazayuni; ambapo hali ya watu wanne imeripotiwa kuwa mbaya.  

Wakati huo huo wanajeshi kadhaa wa Israel wamejeruhiwa katika mapigano ya silaha kati ya wanamuqawama na wanajeshi wa utawala huo katika kambi ya Jenin. Duru za Kizayuni zimeripoti kuwa, jeshi la utawala huo limehuisha mfumo wake wa ulinzi wa anga wa Kuba la Chuma "(Iron Dome) katika mipaka ya kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu likihofia jibu linaloweza kutolewa dhidi yake na wanamuqawama wa Ghaza dhidi ya jinai ya leo huko Jenin.  

4117408

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha